Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Wanasiasa, wasanii waomboleza kifo cha Dk. Mengi
Habari Mchanganyiko

Wanasiasa, wasanii waomboleza kifo cha Dk. Mengi

Spread the love

MAMIA ya waombelezaji wameendelea kumiminika nyumbani kwa Dk. Reginald Mengi Hananasif, Kinondoni, jijini Dar es Salaam kutoa salamu za pole huku wakimuelezea marehemu kuwa aligusa mioyo ya watu wengi. Ananripoti Faki Sosi … (endelea).

Mwili wa Dk. Mengi aliyefariki usiku ya kuamkia tarehe 2 Mei, 2019 jijini Dubai, Falme za Kiarabu, unatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu ya tarehe 6 Mei, mwaka huu na kuagwa Jumanne na kuzikwa Alhamisi kijijini kwao Machame, mjini Moshi.

Tangu taarifa za kifo cha Dk. Mengi zifahamike nchini watu wengi wamekuwa wakituma salamu za pole na kuhudhulia nyumbani kwa marehemu.

Eng. Ester William Mshindi wa Tuzo zinazotolewa na Dk. Mengi wa Walemavu kila mwaka amesema kuwa Dk. amewathamini walemavu kiasi ambacho aliandaa mashindano maalum ambayo hakuna mtu yoyote nchini aliyefikiria kuanzisha tuzo zilizowapandisha thamani walemavu.

“Ametuthamini sana kiasi ambacho kila mwaka amekuwa akiindaa chakula na kula pamoja nasi na akaenda mbali akaanzisha tuzo za ‘ICAN’ kwa ajili yetu,” amesema Eng. Ester.

Ummy Nderiananga, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania amesema kuwa Dk. Mengi atakumbukwa  kwa huruma, upendo na ukarimu wake kwa walemavu.

“Alikuwa na moyo wa kujitolea amejitoa kwa walemavu, amewasaidia watu wengi hapa nchini,” amesema Ummy.

Naye John Malecela, Waziri Mkuu Mstaafu amesema kuwa Dk. Mengi atakumbukwa na watanzania wengi kutokana na wema wake.

“Mengi aliwahi kusema tutakapokuwa tumekufa na tumezikwa kwenye makabuli msitutafute kwenye makabuli yaliyopakwa chokaa mtutafute kwenye mioyo ya wale tuliowahudumia,” amesema Malecela.

SACP Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, amesema Dk. Mengi alikuwa rafiki wa watanzania wote na alikuwa aliyejitofautisha na matajiri wengi.

“Kipato chake hakikuwa kwa ajili ya familia yake tu… alijitofautisha na matajiri wengine kwa kusaidia jamii,” amesema Mambosasa.

Zuwena Mohammedi (Shilole), Mwanamuziki wa Bongo Fleva, amesema kuwa kifo cha Dk. Mengi ni pigo kwa tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

James Mbatia, Mbunge wa Vunjo amesema kuwa Dk. Mengi alimhusia kuchunga wake. “Nilizungumza na Dk. Mengi tarehe 10 Machi, 2019 na alinihusia kuwa maisha yapo kwenye ulimi, ukichunga ulimi wako, ukitumia ulimi wako vizuri utakusaidia kujenga utu, na aliweza kufika alipofika kwa sababu ya ulimi wake.”

Jana na leo tayari watu na kada tofauti tofauti wamefika nyumbani kwa Dk. Mengi kuhani msiba huo, wakiwemo Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, Hashimu Rugwe, Mwenyekiti wa Chama Ukombozi wa Umma, Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Wengine ni Joseph Butiku, Kameshina wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Ole Sendeka, Malecela,  Fahm Dovutwa, Mwenyekiti wa UPDP, Mrisho Mpoto, na Shilole.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

Habari Mchanganyiko

Kairuki awaweka mtegoni wakurugenzi watakaoshindwa kufikia malengo ya makusanyo

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na...

error: Content is protected !!