March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanasiasa wampasua kichwa RPC Mkondya

Lucas Mkondya, Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Spread the love

ALIYEKUWA Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lucas Mkondya, amesema anaondoka katika mkoa huo, huku akisema moja ya changamoto katika nafasi yake ni wanasiasa, anaandika Irene David.

Hata hivyo, hakufafanua alichomaanisha anaposema wanasiasa, lakini hivi karibuni kumekuwapo maneno yanayosemwa na wanasiasa.

Mkondya aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam alipokuwa anawaaga baada ya kuhamishwa katika nafasi hiyo, na kurithiwa na Lazaro Mambosasa.

Changamoto nyingine alizoziacha Dar es salaam ni pamoja na makosa ya barabara na makosa mengine, lakini amejivunia kufanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa uhalifu jijini Dar es Salaam.

Mkondya ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara na leo ameagana na waandishi wa habari.

error: Content is protected !!