January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanasheria wakemea udhalilishaji wa wafanyakazi

Spread the love

BAADHI ya wanasheria mkoani Dodoma wamepinga vikali vitendo ambavyo vinafanywa na baadhi ya watumishi wa serikali kwa kuwaweka wenzao ndani au kuwapiga. Anaandika Dany Tibason, Dodoma …. (endelea)

Wanasheria hao wamelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya viongozi ndani ya serikali kutumia nyadhifa zao kuwapiga au kuwashweka ndani watumishi wa ngazi ya chini.

Mmoja  wa mawakili na Ofisi sheria Modester Mganga kutoka Goldmarc Attorneys Advocates, akizungumza na MwanaHALISI Online alisema siyo sahihi kumchapa,kumfunga mtumishi.

“Hakuna sheria yoyote ambayo inamfanya mtu yoyote ambaye anatakiwa kumpiga mtu kazini au kumdhalilisha kwa kumpiga.

“Kila ofisi ina utaratibu wake na kama kuna kosa lolote ambalo linaonekana kutokea ni lazima taratibu zifuatwe na ni vyema kama mtu amefanya kosa anatakiwa kupewa onyo” na si vinginevyo”amesema Mganga.

Amesema ikumbukwe mkuu wa wilaya ya Bukoba,Albert Mnale aliyewachapa viboko walimu aliachishwa kazi kwani alionekana kuvunja sheria.

Kwa upande wake Wakili Miriam Ndeserua katika Ofisi ya Wasonga Advacates,alisema kitendo cha wakuu wa mikoa,wilaya au wakurugenzi kuwapiga watumishi wa chini yao kwa makosa ya kawaida ni unyanyasaji.

“Amesema hakuna sheria ambayo inampa mamlaka kiongozi yoyote kumpiga mfanyakazi au kumweka ndani kama mtumishi huyo hajafanya kosa la jinai.

“Kila jambo linaendeshwa kwa misingi ya utawala bora kama kuna jambo lolote ambalo mtumishi amelifanya lazima sheria za kazi zifuatwe na kama kuna sababu ya kutoa onyo kwa mdomo au barua zifuatwe”alifafanua Ndeserua.

Amesema kutokana na vitendo hivyo watumishi wa wanaotendewa vitendo hivyo wanatakiwa kufanya taratibu za kuwashitaki wanaowadhalilisha kwa kufuata taratibu za kazi.

Hivi karibuni watendaji wa wa serikali kwa ngazi ya wakuu wa mikoa wakuu wa wilaya wamelalamikiwa kwa kuwashambulia watumishi kwa kuwapiga makofi au kuwaweka rumande kwa kisa cha watumishi hao kuchelewa kazini.

error: Content is protected !!