Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Wanasheria waitaka Serikali kuwachukulia hatua viongozi vyombo vya uokozi
Habari

Wanasheria waitaka Serikali kuwachukulia hatua viongozi vyombo vya uokozi

Spread the love

TIMU ya wanasheria wanaosimamia uwajibijaji wa kimazingira (Lawyers Environmental Action Team -LEAT), imeitaka Serikali kuwachukulia hatua viongozi wa vyombo vya umma vya uokozi na maafa, kwa kushindwa kuwaokoa kwa wakati wahanga wa ajali ya ndege Bukoba, mkoani Kagera. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatatu, tarehe 7 Novemba 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa LEAT, Dk. Rugemeleza Nshala, siku moja baada ya ajali hiyo ya ndege inayomilikiwa na Kampuni ya Precision Air, kutokea.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumapili baada ya ndege hiyo iliyokuwa na watu 43, kutumbukia katika Ziwa Victoria, baada ya kushindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kagera, ikitokea Dar es Salaam, kutokana na hali mbaya ya hewa na kuuwa watu 19 na kujeruhi 24.

Taarifa ya Dk. Nshala imeeleza kuwa, LEAT imeshtushwa na kusikitishwa na udhaifu wa vyombo hivyo kushindwa kufanya majukumu yake mapema, hadi pale wavuvi walipoingilia kati kufanya uokoaji, kama ilivyotokea katika ajali ya Mv. Bukoba 1996.

“Haikutegemewa kuwa miaka 26 tangu ajali mbaya ya Mv. Bukoba, vyombo vyetu vingekuea havijaboresha utendaji wake wa Kazi na kwa kweli havijui kuokoa kwa wakati ajali za ndege na majini zinapotokea. Jana wavuvi wameokoa huku vyombo vya umma vyenye watu wanaolipwa mabilioni Kila mwaka vikiwa having uwezo,” imesema taarifa ya Dk. Nshala.

Taarifa hiyo imesema “LEAT inataka kuwajibishwa kwao mara moja na si kutumia njia za geresha kuunda tume na kamati za uchunguzi na kusema tuendelee kusubiri matokeo. Ukweli ni kuwa, vyombo na mamlaka husika zimezembea kwa kiwango cha aibu kwa Taifa.”

Katika hatua nyingine, taarifa ya Dk. Nshala imesema, LEAT inaitaka Serikali kuboresha Uwanja wa Ndege wa Bukoba, ili kuondoa changamoto zake, ikiwemo tatizo la Hali mbaya ya uwanja wakati wa mvua.

“Tatizo la hali mbaya ya uwanja linafahamika, si mara moja au mbili muonekano dhaifu wa uwanja huo wakati wa mvua limejitokeza na ndege kulazimika kuzunguka juu ya ziwa Victoria na anga ya Bukoba kusubiri hali ya hewa kuboreka. Marubani hulazimika kutumia uzoefu wao kutua katika hali hiyo,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“Ajabu yake mamlaka husika hazijaboresha mfumo wa mawasiliano ya ndege pamoja na kuweka taa za uwanjani ili kuweza kuonekana kwa njia ya uwanja. Na kuwapo kwa mawasiliano ya waongoza ndege wenye mamlaka kuruhusu ndege kutua ama kutotua.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!