August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanaotafuta utajiri kwa nguvu za giza waonywa

Spread the love

WATANZANIA wanaotaka kupata utajiri wa haraka wametakiwa kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuwaingizia kipato badala ya kufanya matambiko yenye kafara za mauaji na unyayasaji ndani yake. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Onyo hilo limetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Maombi na Maombezi kwa Mataifa yote (RUTACH), Living Mwambapa alipokuwa akihubiri kwenye ibada ya katikati ya wiki katika Kanisa hilo lililopo Kikuyu Kaskazini Jijini Dodoma.

Askofu Mwambapa ambaye alikuwa akihubiri katika ibada maalumu ya mafanikio na uimara wa kumtumikia Mungu amesema hakuna mwanadamu ambaye anaweza kupata mafanikio ya kweli kama hatosimama katika ukweli na kufanya kazi kwa uhalali.

Katika ibada hiyo Askofu Mwambapa amewataka waumini wa Kanisa hilo na watanzania kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii ili wapate maendeleo badala ya kufikiria kutoa kafara za kumwaga damu za watu au kufanya ukatili wa kijinsia kama vile, kubaka, kulawiti au kuiba mali za watu.

Kiongozi hiyo ambaye makao makuu ya Kanisa yapo Dodoma amesema ili kuwa matajiri na kuzikimbia kelele na mafundisho ya shetani ni lazima kufanya kazi kwa bidii na kusoma kwa bidii maandiko matakatifu.

“Kwa siku hizi kuna sauti za kila aina na ushawishi mwingi wa kishetani, wapo watu ambao wanatafuta utajiri kwa kudanganywa na waganga ili watoe kafara ya kumwaga damu kwa kuua binadamu mwenzake au kufanya matendo maovu ya ubakaji na wakati mwigine kukimbimbia na viungo vya watu.

“Unyanyasaji na ukatili wa kutisha unafanywa na baadhi ya watu wenye nia na kiu ya kupata utajiri bila kufanya kazi hatari jambo ambalo kinyume na mapenzi ya Mungu” ameeleza Askofu Mwambapa.

Kutokana na kila mmoja kuwa na kiu utajiri kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa bidii na ujue kumtegemea Mungu kwa kila Jambo.

Aidha, kiongozi huyo amewaasa Watanzania kuepukana na matendo ambayo ni machukizo mbele za Mungu watu wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na Mungu ni mwamimifu.

error: Content is protected !!