November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanaoongoza kanda Chadema hawa hapa 

Lazaro Nyalandu, Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Chadema

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewatangaza viongozi wake 29 wa kanda, waliochaguliwa katika chaguzi zilizofanyika kuanzia tarehe 28 Novemba hadi Desemba Mosi mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Viongozi hao, wametangazwa leo tarehe 3 Desemba 2019 na Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema.

Viongozi wa Kanda ya Serengeti ni Esther Matiko, mwenyekiti wa kanda hiyo, wakati makamu wake akiwa Gimbi Massaba, huku mweka hazina akiwa Bernard Makoye.

Ezekiel Wenje amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria, ambapo msaidizi wake ni Sylivester Makanyaga na mweka hazina ni Upendo Peneza.

Kanda ya Pemba inaongozwa na Hafidh Ali Saleh aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kanda hiyo, Time Ali Suleiman, Makamu Mwenyekiti na Ali Khamis Ali, Mweka Hazina.

Said Mzee Said amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Unguja, wakati makamu wake ni Hassan Abeld na Asiata Said Abubakari, Mweka Hazina.

Kanda ya Kusini Mwenyekiti wake ni Seleman Mathew, Makamu Mwenyekiti ni Salum Barwan na Mweka Hazina, Mario Milllinga.

Kanda ya Nyasa itaongozwa na Mchungaji Peter Msigwa (Mwenyekiti), akisaidiwa na Joseph China (Makamu Mwenyekiti) na Mweka Hazina ni Aidan Khenan.

Lazaro Nyalandu, Mwenyekiti wa Kanda ya Kati, wakati Makamu Mwenyekiti akiwa Aisha Luja, na Mweka Hazina ni Devotha Minja.

Kanda ya Magharibi viongozi wakee ni Gaston Garubindi (Mwenyekiti), Masanja Musa (Makamu Mwenyekiti) na Aidan Ndowa (Mweka Hazina).

Hata hivyo, Kanda ya Pwani haina mwenyekiti kufuatia aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo Fredrick Sumaye kushindwa katika kura za ndio au hapana, kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 28 Novemba mwaka huu.

Hivyo, uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa kanda hiyo utarudiwa. Aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti ni Baraka Mwago na Mweka Hazina ni Dk. Michael Mtaly.

error: Content is protected !!