March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanaompinga Rais Mnangagwa watoswa Zimbabwe

Spread the love

MAHAKAMA ya Kikatiba nchini Zimbabwe imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na chama kikuu cha upinzani nchini humo MDC, ya kukata rufaa dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyomuweka madarakani Rais Emmerson Mnangagwa. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Chama Kikuu cha Upinzani nchini Zimbabwe, MDC kikiongozwa na aliyekuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi uliofanyika wiki kadhaa zilizopita, kilikwenda mahakamani kupinga matokeo hayo kikidai kuwa yalilenga kumpendelea Rais Mnangagwa.

Uamuzi huo wa mahakama ulitolewa na Jaji Mkuu, Luke Malaba leo Ijumaa tarehe 24 Agosti, 2018 baada ya MDC kushindwa kuithibitishia mahakama hiyo kuhusu udanganyifu uliofanyika kwenye uchaguzi huo.

Katika uchaguzi huo, Rais Mnangagwa kutoka chama tawala cha ZANU-PF alishinda kwa ushindi mwembamba wa asilimia 50.8 ya kura huku aliyekuwa mpinzani wake wa karibu Chamisa akiambulia asilimia 44.3 ya kura wakati asilimia zilizosalia zikichukuliwa na wagombea wa vyama vingine walioshiriki uchaguzi huo wa urais.

error: Content is protected !!