Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wanaolalamika mahindi kupanda, walime ya kwao – Rais Magufuli
Habari za Siasa

Wanaolalamika mahindi kupanda, walime ya kwao – Rais Magufuli

Mahindi
Spread the love

RAIS John Magufuli amewataka watu wanaolalamika bei ya mahindi kupanda, wakalime ya kwao, ili yawe ya bei ya chini. Anaripoti Regina Mkonde … (endela).

Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo tarehe 20 Novemba 2019, wakati akizungumza na wananchi mkoani Morogoro.

“Ukiona wengine wachache wanalalamika bei ya mahindi iko juu, na nataka wakulima washangilie zaidi. Tulizungumze hili wazi, kwa Watanzania wote, ukiona mahindi yako juu, nenda kalime yako ya bei ya chini, biashara hii lazima iwe huru,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema katika uongozi wake, hatawapangia bei wakulima, kwa kuwa anafahamu shida wanazopitia wakati wa kulima na hata kuvuna mazao yao.

“Katika kipindi changu sitapanga bei ya mkulima, na mimi ni mtoto wa mkulima ninafahamu maana ya kulima, sasa wale wanaotaka bei nzuri ya mazao, huu ndio wakati kutengenza bei nzuri, mvua zimeanza kunyesha na wewe ukawe na kashamba kako,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;

“Mkulima anatafuta mbolea, anahangaika kule anafukuzana na nyoka matope ni yake,wakati wa kuvuna ni yeye,halafu avune umpangie bei..bei itajipanga yenyewe,wakati wa kuwapangia bei wakulima mazao yao umeshakwisha.”

Kauli hiyo ya Rais Magufuli imekuja kukiwa na malalamiko ya bei ya baadhi ya bidhaa kupanda, ikiwemo unga wa mahindi.

Hivi karibuni Dk. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akiwa bungeni jijini Dodoma, alisema bei ya bidhaa za chakula ikiwemo unga wa mahindi, imepanda kutokana na baadhi ya maeneo hayakupata chakula cha kutosha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!