February 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wakiukaji sheria, utaalamu mipangomiji kukiona

Spread the love

WILLIAM Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameitaka bodi ya usajili wa wataalamu wa mipangomiji kuwachukulia hatua wataalamu wa mipangomiji wanaotumia jina la halmashauri kutekeleza kazi za kampuni binafsi, anaandika Hamisi Mguta.

Lukuvi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akisoma hotuba yake katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu wa mipangomiji.

Amesema wataalamu hao ambao ni waajiliwa wa halmashauri wanaofanya kazi na sekta binafsi (makampuni) kwa kutumia jina la halmashauri wanazofanyia kazi ili kazi za kampuni zionekane kua ni za halmashauri.

“Hili ni kosa kisheria, kwasababu wanasababisha sekta binafsi katika upangaji miji kutoonekana wazi, lakini pia wanaikosesha serikali mapato hivyo ni vyema kutambua kua kulipa kodi ni wajibu wa kila mtu na taasisi husika,” amesema.

Amesema, amepata taarifa kua kuna taasisi za umma zikiwemo baadhi ya halmashauri, sekta binafsi na asasi zisizo za kiserikali zinawatumia wataalamu hao au kampuni za upangaji ardhi zisizosajiliwa kufanya kazi ya upangaji wa ardhi ambayo ni kinyume na sheria.

“Bodi ichukue hatua za kisheria kukomesha hali hiyo kwa kuwafungulia mashitaka wale wanaokiuka sheria hata kama ni taasisi za umma,”amesema.

Aidha, amesema kwakua sekta ya ardhi ni sekta nyeti ya taifa na yakila mwananchi hivyo bodi ambayo ndio imepewa jukumu la kusimamia rasilimali hiyo lazima ihakikishe inaweka mipango mizuri kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

“Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ‘Ili tuendelee tunahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora’ hivyo mipango ya matumizi ya ardhi ni lazima,”amesema.

 

error: Content is protected !!