January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wanaoharibu mazingira washughulikiwe’

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akizindua ripoti ya hali ya mazingia.

Spread the love

MAKAMU wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amezindua ripoti ya pili ya hali ya mazingira nchini ya mwaka 2014, na kuziagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua waharibifu wa mazingira. Anaripoti Sarafina Lidwino…(endelea).

Akizungumza katika tukio hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge amesema, hii ni ripoti ya pili kutengenezwa tangu ile ya mwaka 2008.

Amesema, kuchelewa kwa uchapushwaji wa ripoti hii kumetokana na uhaba wa rasilimali fedha zinazohitajika katika mchakato mzima wa kuandaa ripoti ya namna hiyo.

Mahenge ameongeza “tumebaini kipindi cha miaka miwili ni kifupi hasa katika kubainisha mabadiliko katika mwenendo wa mazingira nchini.”

“Kwa kuwa suala hili ni la kisheria, tunakusudia kushirikiana na wadau mbalimbali. Hivyo, tunachukua fursa hii kwa kuomba muda ubadilishwe ili tupate muda wa kutosha wa kuweza kubaini mabadiliko ya mwenendo wa hali ya mazingira,” amesema Mahenge.

Amesema, ripoti hiyo imefanya utafiti wa kina kuhusu masuala yanayosababisha uharibifu na mabadiliko katika mazingira. Maeneo yaliyofanyiwa tathmini ni kilimo, misitu, bioanuai na rasilimali za maji.

“Tumebaini kuwa pamoja na kuwepo kwa jitahada mbalimbali za kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira nchini, bado hali ya mazingira imeendelea kutoridhisha,” amesema Mahenge.

Naye Dk.Bilal baada ya kuzindua ripoti hiyo, amesema, “changamoto tumezisikia na niwaahidi kuziagiza sekta husika kupitia upya sheria na sera za misitu ili kupambana nazo. Nawale wanaoharibu mazingira kwa makusudi kama kuchoma moto kiholela, naagiza wizara husika iwashughulikie.”

error: Content is protected !!