Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanaohama Ngorongoro: Majaliwa atoa maagizo wizara 4
Habari MchanganyikoTangulizi

Wanaohama Ngorongoro: Majaliwa atoa maagizo wizara 4

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameitaka wizara ya maliasili na utalii kuendelea kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha shughuli za ujenzi katika kijiji cha Msomera kilichopo Handeni mkoani Tanga zinakamilika haraka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Amesema wizara hiyo inapaswa kuhakikisha inaendelea kutoa elimu kwa wakazi wa Ngorongoro waliojiandikisha kuhama kwa hiari.

“Zoezi hili linaloendea la kuimarisha miondombinu ikiwemo upimaji wa viwanja litawanufaisha wakazi wa Msomera pamoja na hao wanaohamia eneo hili,” amesema.

Majaliwa alisema hayo jana Jumapili, tarehe 24 Aprili 2022, alipokagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika kijiji cha Msomera kilichopo Handeni kwa ajili ya wakazi wa Ngorongoro waliokubali kuhamia kwenye Kijiji hicho ili kupisha shughuli za uhifadhi kwa maendeleo ya Taifa.

Aidha, Majaliwa ameitaka wizara ya mifugo na uvuvi kuendelea kuandaa mazingira mazuri ya ufugaji.

“Wizara hii inapaswa pia kuhakikisha kwamba kunakuwa na miundombinu wezeshi ya wafugaji yakiwemo malambo ya kunyweshea mifugo, majosho, ujenzi wa kliniki ya kutibu magonjwa ya mifugo katika eneo hilo,” amesema.

Akitoa maelekezo kwa Ofisi ya Rais-Tamisemi, Majaliwa ameitaka iendelee kuwekeza nguvu katika kuimarisha miundombinu ya elimu.

“Kama tunavyoona hapa shule ya msingi inajengwa, sekondari inajengwa, zahanati zinakarabatiwa lakini pia ujenzi wa kituo cha afya na barabara unaendelea, ongezeni nguvu,” alisema

Majaliwa pia ameitaka wizara ya maji iendelee kuhakikisha kiwango cha maji katika eneo hilo kinakuwa toshelevu kwa kuchimba zaidi ili hata majosho na malambo yapate maji ya kutosha. Maji ambayo tayari yameshachimbwa na kuyapata ni mengi kuliko mahitaji lakini tuongeze kiwango.”

Pia, Waziri Mkuu alisema watumishi wote wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) waliojenga katika hifadhi ya Ngorongoro hawataingia kwenye utaratibu wa kupewa nyumba kwa kuwa walivunja sheria.

“Nataka niwaambie watumishi wa NCAA mliojenga kule, tutaondoa nyumba zenu zote kwasababu mmevunja sheria, kama unajua umejenga anza kuondoka mwenyewe,” alisema.

Kwa upande wake, waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Angelina Mabula amesema wizara ilipokea shilingi milioni 321 kwa ajili ya kufanya mpango wa matumizi bora ya ardhi katika kijiji cha Msomera na mpaka sasa jumla ya michoro 11 imeshakamilika ambapo michoro mitano tayari ina viwanja 14,250 na katika hivyo viwanja 5,250 tayari viko kamili.

Alisema wakazi hao watapewa viwanja hivyo bure, “tunatarajia kijiji hiki kitakuwa cha mfano na hata vijiji vingine vitakuja kujifunza hapa. Tulichokifanya kama wizara ni kuhakikisha mpango wa matumizi bora unakamilika.”

Naye, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema wizara hiyo itahakikisha miradi yote ya maji katika kijiji cha Msomera inakamilika kwa wakati ili wakazi hao waweze kupata huduma ya maji safi na salama.

“Kupitia Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) tunakwenda kuchimba bwawa ambalo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 700 na tayari tumekamilisha hatua za manunuzi na mkataba imeshasainiwa tumeshaleta shilingi milioni 300 ili kazi iendelee na wakandarasi wote wa Wizarani wapo hapa.”

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki alisema Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya uejnzi wa majosho mawili mapya na ukarabati wa josho moja lililopo katika kijiji hicho, “ Tunazo pesa na tayari wataalam wetu wapo hapa wapo tayari kushikiana nanyi ili kubaini ni wapi mnataka majosho hayo yajengwe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

error: Content is protected !!