Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanaobambikizia kesi wananchi kukiona
Habari Mchanganyiko

Wanaobambikizia kesi wananchi kukiona

Suleiman Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Spread the love

SELEMANI Jafo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kuchukua hatua dhidi ya watendaji wa serikali wanaowabambikia kesi wananchi, anaandika Dany Tibason.

Jafo alikuwa akijibu swali la Dk. Dalaly Kafumu, Mbunge wa Igunga, Tabora aliyedai kuwa wananchi hususan wa vijijini wamekuwa wakisingiziwa makosa mbalimbali na watendaji wa serikali kutokana na uelewa mdogo wa masuala ya kisheria na haki zao.

Dk. Kafumu aliwatuhumu watendaji wa vijiji na kata ambao alidai wamekuwa wakishirikiana na mahakimu wa mahakama za mwanzo na mabaraza ya ardhi kuwaonea na kuwadhulumu wananchi ikiwemo kuwabambikiza kesi na kuwanyang’anya ardhi.

“Je, ni lini Serikali itachukua hatua za kukomesha tabia hiyo?” alihoji Dk. Kafumu.

Akijibu swali hilo, Jafo alikiri kuwepo na malalamiko dhidi ya baadhi ya watendaji wa kata na vijiji na hivyo kuwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya wahakikishe wanasimamia maadili ya watendaji  kwa ngazi zilizo chini yao na kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanaobambikizia kesi wananchi.

“Watendaji wote katika ngazi zote za mamlaka za Serikali za Mitaa wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji  wa majukumu yao, Serikali haitasita kumchukulia  kali mtendaji atakaekiuka sheria, kanuni na taratibu za kazi,” amesema.

Naibu Waziri huyo amesema Serikali itaendelea kuhakikisha inasimamia kikamilifu maadili  ya watumishi wa umma kwani ndiyo msingi wa usatawi wa jamii na kwamba hakuna mtumishi wa umma asiye na maadili atakayevumiliwa.

“Nato wito kwa viongozi na wananchi wote nchini kuhakikisha wanawafichua watendaji na watumishi wa umma wenye tabia kama hii ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!