Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wananchi wazidi kuikimbia Gambia
Kimataifa

Wananchi wazidi kuikimbia Gambia

Rais Yahya Jammeh anayeikalia Gambia kwa mabavu
Spread the love

HALI ya taifa la Gambia inazidi kuwa tete. Utawala wa mabavu wa Rais Yahya Jammeh umesababisha sintofahamu kubwa huku raia wakichukua tahadhari ya kuanza kuikimbia nchi hiyo, anaandika Wolfram Mwalongo.

Sheriff Bojang Waziri wa habari nchini Gambia pia amekimbilia uhamishoni nchini Senegal, ikiwa ni wiki moja tangu Shirika la Habari la Uingereza (BBC) kuripoti kukimbia kwa Alieu Momar Njai Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Gambia.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema kinachoendelea ni dalili ya anguko la taratibu la utawala wa Rais Jammeh ambaye amekuwa king’ang’anizi madarakani – akigomea matokeo ya uchaguzi wa Desemba mosi mwaka jana yaliyomuangusha.

Hata hivyo jitihada za kumtaka kiongozi huyo wa Gambia kutii Katiba ya nchi hiyo zimeendelea kufanyika chini ya Rais Muhammadu buhari wa Nigeria.

Idadai ya raia wa taifa hilo wanaoingia nchi jirani ya Senegal imekuwa ikiongezeka kutokana na hofu ya kuibuka kwa machafuko baada ya tarehe 19 Januari, 2017 huku wafuasi wa Rais mteule Adama Barrow wakisema endapo Rais Jammeh aliyemaliza muda wake hataondoka Ikulu watamuita muasi.

Tayari Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas), imemtahadhalisha rais huyo huku ikiahidi kumtoa madarakani kwa “mtutu” endapo hataheshimu maamuzi ya wananchi wa Gambia, waliomkataa kupitia sanduku la kura Desemba mosi mwaka jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!