January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi waua polisi Mwanza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola

Spread the love

MATUKIO ya wananchi kujichukulia sheria mikononi yanazidi kuchukua sura mpya baada ya askari Polisi PC Magesa kushambuliwa na kisha kuuwawa katika Mtaa wa Kanindo Kata ya Igoma Wilayani Nyamagana Mkoa wa Mwanza.

Taarifa zilizolifikia MwanahalisiOnline, zimedokeza kuwa, askari huyo aliuawa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya wizi.

Tukio hilo la kinyama limetokea juzi usiku, ambapo marehemu anadaiwa kukutwa akifanya uhalifu pamoja na wenzake wawili pamoja na askari mgambo, ingawa watuhumiwa hao majina yao hayakufahamika mara moja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola amethibitisha tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa kamili kesho.

error: Content is protected !!