August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi waua majambazi Dodoma

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam

Spread the love

WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuwawa na wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Dabalo Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma wakidaiwa kuvamia kijiji hicho ili kupora fedha, anaandika Dany Tibason.

Katika tukio hilo pia majambazi wawili walikamatwa na mpaka sasa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi ambapo wanatarajia kufikishwa mahakamani huku jambazi mmoja akifanikiwa kutoroka katika eneo la tukio.

Lazaro Mambosasa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 21 Desemba mwaka huu majira ya saa tatu usiku.

“Baada ya majambazi kuvamia na kuanza kufanya unyang’anyi katika kijiji cha Dabalo taarifa zilienea vijiji vya jirani ambapo wananchi waliamua kufunga barabara huku wakiwa na silaha za jadi ambapo walifanya msako mkali katika mapori.

Majambazi waliona tochi za makundi ya wanakijiji huku wakiwa wamewazunguka na kufanya mashambulizi kwa silaha za jadi, ndipo baadhi walipouawa baada ya kuamua kuzitelekeza pikipiki zao na kukimbilia katika mlima wa Kinyami uliopo kijiji cha Hombolo,” amesema.

error: Content is protected !!