Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wananchi watawanywa kwa mabomu ya machozi Arumeru
Habari za Siasa

Wananchi watawanywa kwa mabomu ya machozi Arumeru

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, (RPC), Charles Mkumbo
Spread the love

MGOGORO wa kugombea mpaka kwa wakaazi wa Kijiji cha Momella, Kata ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru na Hifadhi ya Taifa ya Arusha (Anapa) umechukua sura mpya baada ya polisi kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wananachi kuwazuia wasiandamane, anaadika Mwandishi Wetu.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki baada ya wananchi hao kukusanyika kwa makundi kwa lengo la kuandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kupinga kitendo cha hifadhi hiyo kuweka alama za mipaka ndani ya maeneo wanayoishi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mwenyekiti wa Kitongoji cha Momella, Anaeli Nko, amesema hivi karibuni polisi walifika kijijini hapo wakiwa na silaha za moto ambapo ghafla walianza kuwatawanya wananchi kwa kuwapiga mabomu ya machozi.

Huku akionyesha maganda ya risasi za mabomu ya machozi yaliyopigwa siku hiyo Nko amesema, baadhi ya wananchi walikamatwa na kisha kupelekwa katika kituo cha polisi cha Usa River huku akisema wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakiishi kwa hofu ya kukamatwa na polisi jambo ambalo limepelekea kudumaza maendeleo yao.

Naye Mwenyekiti wa Tawi la CCM kijiji cha Momella, Godfrey Urio, amesema mgogoro wa kugombea mipaka baina ya kijiji chao na hifadhi ya Anapa ni wa muda mrefu na wanashangaa kwa nini serikali imeshindwa kuingilia kati kuutatua.

Amesema hivi karibuni hifadhi hiyo ilivamia ndani ya kijiji chao na kuweka alama mbalimbali za mipaka kitendo ambacho kinaashiria ya wao wanastahili kuondoka katika maeneo ambayo mipaka hiyo imewekwa.

Mkazi wa kijiji hicho, Mage Hudson, amesema polisi waliingia na kupiga mabomu ya machozi wakati wakiwa kwenye ibada na kudai wanashangaa serikali kuthamini wanyama badala ya binadamu.

“Watu wa Anapa wanathamini wanyama badala ya binadamu sisi tuna zaidi ya miaka 60 tunaishi hapa wengi tulizaliwa na kukulia hapa hapa na hata makaburi ya wazazi wetu yako hapa hapa,” amesema Hudson Sabason.

Akizungumzia sakata hilo amesema pamoja na tume mbalimbali kuundwa kuutatua mgogoro huo lakini bado wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakinyanyasika huku akisisitiza kwamba askari wa hifadhi wamekuwa wakipita ndani ya kijiji chao na kuwatolea vitisho.

Naye, Elizabeth Luka amesema wamekuwa wakiishi ndani ya eneo hilo tangu mwaka 1945 na wanashangaa sasa kuamriwa waondoke kwa madai wanaishi ndani ya eneo la hifadhi na kuiomba serikali iingilie kati mgogoro huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, (RPC), Charles Mkumbo, alithibitisha polisi kuwatawanya wananchi kwa mabomu ya machozi kwa sababu za kiusalama.

Hata hivyo, Mkumbo amesema hivi karibuni kwenye ziara ambayo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuutatua mgogoro huo huku akisisitiza hakuna mwananchi atakayekamatwa katika kijiji hicho kwa kuwa suala hilo linaahughulikiwa katika ngazi ya mkoa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

Habari za Siasa

Dorothy Semu ajitosa kumrithi Zitto ACT-Wazalendo

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, anayemaliza muda wake, Dorothy...

error: Content is protected !!