January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi watakiwa kutoa taarifa za mafisadi

Spread the love

MKURUGENZI wa Mashitaka nchini DPP, Biswalo Mganga amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi na upelelezi kwa kutoa taarifa za kweli juu ya watu ambao wanafanya makosa ya uhalifu wa kifedha. Anaandika Regina Mkonde … (endelea) .

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema jeshi la polisi litahakikisha linatunza siri za watoa taarifa kulinda usalama wao na kuwatoa hofu kwa kuwapa ushirikiano unaotakiwa.

“Jeshi la Polisi litazifanyia kazi taarifa zote za kihalifu zitakazotolewa na wananchi wema, na litatunza siri hizo kwa manufaa ya usalama wao pamoja na taifa zima kwa ujumla

Amesema katika operesheni hiyo wanalenga kutaifisha mali zote zilizopatikana isivyo kihalali zitataifishwa na kurudishwa serikalini na wahusika watafikishwa mbele ya sheria.

Amesema kazi hii haiwezi kufanywa na Jeshi la Polisi na TAKUKURU pekee bali kwa ushirikiano wa wananchi ambao ni jeshi kubwa linaloishi karibu na wahalifu hao huko mitaani.

Amesema mwananchi atakae wasaidia wahalifu kuficha ushahidi dhidi ya uhalifu walioufanya serikali itahakikisha nao wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kufunguliwa mashitaka

Amesema wananchi wanapaswa kuachana na masuala ya kihalifu kwani watu wengi wamepoteza maisha kwa kujihusisha na masuala ya kihalifu, wengine kupata vilema vya kudumu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai Diwani Athumani am esema hatua iliyofikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika kupambana na uhalifu ni wa kuridhisha.

Amesema wananchi hawana budi kuziunga mkono taasisi zote zinazo pambana na rushwa hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha janga hili linatokomezwa kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na mdudu rushwa kwa garama yoyote hile bila ya kuogopa vitisho toka kwa taasisi yoyote ndani au nje ya nchi.

Amesema watumishi wote ndani na nje ya hawana budi kuichukia rushwa toka ndani ya mioyo yao kwa maslahi ya taifa bila ya kujali itikadi ya vyama, kinachotakiwa ni uzalendo wan chi kwanza.

error: Content is protected !!