January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi watakiwa kupima afya

Spread the love

WANANCHI wametakiwa kupima afya zao ili kupunguza visababishi vya maradhi mbalimbali ikiwemo saratani. Anaandika Regina Mkonde.

Kauli hiyo imetolewa leo na Dk. Ulisubisya Mpoki ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa niaba ya Waziri wa Afya Dk. Ummy Mwalimu.

Dk. Mpoki amesema ugonjwa wa saratani huathiri watu wa rika na jinsia zote hivyo hauna budi kudhibitiwa ili kukinga athari zake.

“Takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kwamba, kila mwaka duniani kunatokea wagonjwa wapya wa saratani wanaokadiriwa kufikia milioni 14.1.

Kati yao, zaidi ya wagonjwa milioni 8.2 hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani,” amesema Dk. Mpoki.

“Nchini Tanzania tatizo la saratani limekuwa likiongezeka kila mwaka, takribani wagonjwa wapya wapatao 44,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali. Hii ni sawa na asilimia 10 (4,400) kati ya wagonjwa wote wanaofanikiwa kufika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Asilimia 80 ya wagonjwa hao hufika wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa,” ameongeza.

error: Content is protected !!