March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi watakiwa kupima afya zao mara kwa mara

Dk. Faustin Ndungulile

Spread the love

IKIWA leo tarehe 4 Februari 2019 dunia inaadhimisha siku ya saratani, serikali imeendelea kusisitiza wananchi kupima afya zao ili kukabiliana na ugonjwa huo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 4 Februari 2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulie.

Dk. Ndugulile ameeleza kuwa, watanzania wengi wenye ugonjwa wa saratani huchelewa kufika hospitali kwa ajili ya matibabu kitendo kinachopelekea kukosa tiba kwa wakati na kufariki dunia.

Amesema, takribani watu 55,000 hupata ugonjwa wa saratani kila mwaka, ambapo wanaowahi kufika hospitali kwa ajili ya vipimo na matibabu ni asimilia 25 pekee, huku asilimia 70 wakifika katika hatua za mwisho.

“ Watu 55,000 hupata saratani kwa mwaka, asilimia 25 wanawahi kufika, asilimia 70 wanafika wakiwa wamechelewa. Tunawataka Watanzania kujitokeza kwa wingi sababu kupima ni bure,” amesema Dk. Ndugulile.

error: Content is protected !!