August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi watakiwa kukipa ushirikiano kikosi kazi

Spread the love

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe amewasilisha maoni ya Wizara hiyo kwenye kikosi kazi cha Rais Samia Suluhu Hassan, huku akiwataka Watanzania watakaofikiwa na kikosi hicho watoe ushirikiano. Anaripoti Selemani Msuya … (endelea).

Prof. Shemdoe amesema hayo leo tarehe 5 Julai, 2022 baada ya kumaliza kutoa maoni ya Wizara ya TAMISEMI kwa kikosi hicho jijini Dar es Salaam ambapo alisema ana imani maoni yao yarafanyiwa kazi.

Alisema pamoja na mambo mengine, pia wamewasilisha maoni kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unasimamiwa na wizara yao.

“Tunashukuru na sisi tumepewa fursa ya kuwasilisha maoni yetu kwenye kikosi hiki cha kidemokrasia, wetupokea na tunaamini watafanyia kazi maoni yetu,”alisema.

Katibu Mkuu huyo alisema suala la uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ni mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa kwa muda hivyo wametoa maoni yao katika eneo hilo.

Aidha, Shemdoe ametoa wito kwa wananchi ambao watapata fursa ya kukutana na kikosi kazi hicho wawe huru kutoa ushirikiano ili maoni yao yafanyiwe kazi.

Alisema kinachofanywa na kikosi hicho ni kwa ajili ya Watanzania hivyo hawana budi kutoa maoni juu wanachotaka kiwe kwenye mchakato huo.

“Sisi TAMISEMI tumetoa maoni yetu kwa uhuru kabisa naomba na wananchi wajitokeze kutoa maoni yao iwapo watapata fursa hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi,”alisema.

Alisema imani yake ni kwamba yote ambayo watoa maoni wanatoa yatapokelewa na kufanyiwa kazi.

error: Content is protected !!