May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi wapanga kuandamana kumng’oa diwani

Spread the love

 

WAKAZI wa Kata ya Nzuguni Jijini Dodoma wamepanga kuandamana hadi kwa Diwani wao, Mzee Aloyce (CCM) ili wamshinikize kujiuzulu kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodma … (endelea).

Wakizungumza na mwandishi wetu leo tarehe 7 Mei, 2022, wananchi hao wamesema licha ya kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa kuchangishana fedha, bado diwani huyo haoneshi ushirikiani wowote.

Wamesema fedha hizo wamekuwa wakichangisha mathalani kwa matengenezo ya barabara lakini diwani ameshindwa kushirikiana nao.

Hata hivyo, wamesema kwa muda mrefu  kiongozi huyo hafanyi mikutano  na wananchi wake ili kusikiliza kero zao.

“Kwa kipindi kirefu kata ya Nzuguni ambayo ipo umbali wa Kilomita tano kutokea katikati ya Jiji la Dodoma imekuwa kero kwa wananchi kwa kuwa imeharibika.

“Lakini pia kata yetu haina maji safi na salama, cha ajabu diwani yupo tu wala haoneshi jitihada ziozote za kushughulikia matatizo yetu,” amesema mmoja wa wananchi.

Alipoulizwa diwani huyo kuhusiana na tuhuma hizo, alisema malalamiko hayo ya wananchi hayana ukweli wowote, labda ni ajenda binafsi za mtu kumwelekea diwani.

“Ushirikiano gani ambao wanautaka? Nimeitisha mkutano wananchi wamejitokeza wachache, tunajenga daraja, tumeomba barabara na tumepata na zitaanza kutengeneza hivi karibuni. Kama wana ajenda zao na diwani waseme, waje Nzuguni waone kinachofanyika,” alisema Diwani Mzee.

error: Content is protected !!