Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Wananchi waonywa matukio moto hifadhi za misitu
Habari Mchanganyiko

Wananchi waonywa matukio moto hifadhi za misitu

Misitu ya Sao Hill, iliyoko Mufindi mkoani Iringa
Spread the love

WANANCHI waishio pembezoni mwa hidhafi ya msitu wa shamba la miti la Saohill wameonywa kuacha uvamizi mpya wa maeneo ya hifadhi ambao husababisha matukio ya moto katika mashamba hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea)

Onyo hilo lilitolewa jana Jumanne tarehe 9 Septemba 2020 na Afisa Misitu Mwandamizi wa shamaba la misitu Sao Hill, Joseph Sondi katika kikao kazi kilichowakutanisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Maafisa Tarafa na Watendaji wa Vijiji 60 vinavyozunguka shamba la Miti Sao Hill kutoka Wilaya ya Mufindi.

Sondi alisema kutokana na matukio ya moto kukithiri katika miaka ya hivi karibuni ndani ya shamba hilo, wanataka wananchi waache uvamizi mpya wa maeneo ili kudhibiti matukio hayo.

“Ili kudhibiti matukio ya moto mashambani, wakulima wanatakiwa kuimarisha barabara za kinga moto kuzunguka shamba na kuwa na maandalizi ya mashamba yenye umakini,” alisema Sondi

Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Joseph Mchina alisema kikao kimelenga kukumbusha viongozi kuhusu matumizi ya moto yasiyofuata utaratibu ambayo yamekua yakileta hasara kubwa kwani huteketeza mali za wananchi na kupoteza pato la taifa.

Alisema ni vyema wananchi wakaendelea kuchukua tahadhari hasa katika msimu huu wa kiangazi ambapo wananchi wengi wanaanza kuandaa mashamba na kusababisha uanzishwaji wa moto bila kufuata utaratibu.

“Semina hii ni muhimu sana wakati huu ambapo ni msimu wa kiangazi na tunakabiliwa na majanga ya moto na hatari kubwa kwenye tasnia ya misitu ni majanga ya moto.”

“Katika miaka mitatu iliyopita tuliona majanga ya moto yamepungua katika Wilaya yetu,”alisema

“Mwaka jana, tumeona kuna ongezeko la majanga ya moto na halikuwa ongezeko ndogo lilikuwa kubwa na lilitushtua kidogo, sasa ni muhimu kutafakari na kujitathimini kwanini majanga ya moto yaliongezeka na hivyo ni muhimu kwa watendaji kuchukua tahadhari katika kusimamia mashamba ya wananchi na ya serikali.” alisisitiza.

Naye Muhifadhi Mkuu wa shamba hilo, Juma Mwita aliwata wananchi kuthamini misitu iliyorithishwa kwa kizazi cha sasa kwani ina manufaa makubwa kwa jamii ambapo imefanya wananchi wengi kupanda miti kwaajili ya kujiongezea kipato na kuboresha mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

error: Content is protected !!