January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi waonywa kushabikia vyama

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva

Spread the love

WANANCHI wametakiwa kuwachagua viongozi wenye nia ya kupeleka maendeleo kwao na sio kuchagua viongozi kwa ushabiki wa vyama. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo na mgombea wa udiwani katika Kata ya Kilimani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Neema Mwaluko alipokuwa akiomba kupitishwa katika kura za maoni kupitia chama hicho.

Neema amesema, mtu yoyoye ambaye amaomba nafasi ya kuchaguliwa na wakati huo anatoa rushwa achaguliwe kamwe hawezi kuwatumikia wananchi.

Akizungumzia Kata ya Kilimani ameeleza kuwa, kata hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tatizo la kutokupimiwa viwanja jambo ambalo ni tatizo la muda mrefu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Neema amesema, anawaomba wananchi wampitishe katika kura za maoni aweze kuwania nafasi ya udiwani katika kata hiyo ili akabiliane na changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili kata hiyo.

Wananchi wa kata hiyo wamemlalamikia Haruna Kifimbo kwa kuwatumia vijana kuuliza maswali ambayo yanagusa maisha ya mtu binafsi.

Kifimbo ni maarufu kwa jina la Dk. Kifimbo ambaye naye ni mmoja wa wanaoomba ridhaa ya kupitishwa katika kura za maoni kuwani nafasi hiyo ya udiwani.

Wananchi hao wamesema, mara nyingi Dk. Kifimbo amekuwa ikawatumia vijana kwa kuwanunulia viroba vya pombe ili kuvuruga mikutano na kuuliza maswali ambayo hayaendani na masuala ya maendeleo.

Kwa kile ambacho kilonekana kuendelea kuwakera wananchi kutokana na vijana kutaka kuuliza maswali huku wakiwa wamelewa, Katibu Mwenyezi Kata ya Kilimani CCM, Lucy Rutainulwa aliingilia kati na kuwakemea vijana hao kuacha kuuliza maswali ya ovyo.

Kiongozi huyo amesema, kitendo cha vijana kujitokeza na kuuliza maswali huku wakiwa wamelewa au kuuza maswali ambayo yanagusa maisha ya mtu binafsi hayajengi chama.

Dk. Kifimbo amekana kushiriki njama hizo za kuwanunulia viroba vijana ili kuwashawishi waulize maswali ya ovyo au kuvuruga mkutano.

error: Content is protected !!