Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi wanufaika na mkaa endelevu
Habari Mchanganyiko

Wananchi wanufaika na mkaa endelevu

Mkaa endelevu
Spread the love

WANANCHI wa vijiji 22, wazalishaji mkaa maarufu kama mkaa endelevu na Halmashauri za wilaya wamenufaika kwa kupata fedha zaidi ya Sh. 3 bilioni kufutia uvunaji wa mkaa endelevu katika kipindi cha miaka mitano. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Meneja mradi wa mradi wa Kuleta Mageuzi Katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) maarufu ‘mkaa endelevu,’ Charles Leonard alisema wakati akiwasilisha mada kwa maofisa mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Serikali Kuu walikutana mkoani Morogoro.

Meneja huyo alisema mradi wa TTCS unatekelezwa katika vijiji 30 vya wilaya za Mvomero, Kilosa na Morogoro chini ya usimamizi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Kusimamia Misitu Tanzania (Mjukita), Shirika la Kuendeleza Nishati Asili Tanzania (TaTEDO) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC).

Alisema katika mradi huo vijiji 22 vimeanza kunufaika katika pande mbili ambazo ni kiuchumi na utunzaji wa mazingira huku nane vikiwa katika mchakato.

Alisema hadi kufikia mwezi Mei 2019 vijiji vimeweza kikusanya mapato halali zaidi ya Sh. 1.4 bilioni, wachomaji mkàa Sh. 1.2 bilioni na halmashauri Sh. 500 milioni.

Meneja alitaja baadhi ya vijiji ambavyo vimenufaika na mradi ni Ulaya Mbuyuni, Matuli, Kitunduweta, Mlilingwa, Ulaya Kibaoni, Diguzi na vingine.

Leonard alisema mradi wa mkaa endelevu ulianza Machi 2012 katika vijiji 10 lakini baada ya kuonekana mafanikio wamelazimika kuongeza vijiji hadi kufika 30.

“Mradi wa TTCS maarufu mkaa endelevu umefanya mapinduzi makubwa kiuchumi, kijamii na maendeleo katika vijiji vilivyopo kwenye mradi kama kuboresha sekta ya afya, elimu, maji, kilimo na mitaji,” alisema.

Alisema mafanikio ya mradi yamezingatia kutoa elimu kwa jamii husika, watendaji na wafanya maamuzi hivyo kurahisisha utekelezaji.

Meneja alisema pia utekelezaji unazingatia uwepo wa mpango wa matumizi bora ya ardhi za vijiji, kutenga maeneo madogo ya mradi na kuvuna kwa kutumia vitalu.

Alisema pia mradi umefanikisha ujenzi wa ofisi za vijiji hali ambayo inarahisisha usimamizi wa mradi.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa TFCG, Bettie Luwuge alisema warsha hiyo ya siku tatu imelenga kujenga uelewa kwa pande zote ili kurahisisha utunzaji wa misitu nchini.

Luwuge alisema rasilimali misitu ikitunzwa kwa ushirikiano wa wadau wote inaweza kubadilisha jamii kiuchumi na maendeleo.

“Tumeamua kukutanisha maofisa kutoka sekta ya kilimo, misitu, maliasili na sheria wa wilaya 19 lengo ni kuweza kubadilishana mawazo namna ya kutunza misitu yetu ili iwe endelevu,” alisema.

Alitaja wilaya husika kwa warsha hiyo ni Kigoma, Kilwa, Tabora, Namtumbo, Handeni, Kilindi, Mvomero, Morogoro, Kilosa, Lindi, Liwale, Tunduma, Kilolo, Ruangwa, Nachingwea, Mpwapwa, Songea, Nyasa, Mbinga.

Awali akifungua warsha hiyo Ofisa Misitu wa Mkoa wa Morogoro, Joseph Chuwa alisema warsha hiyo itasaidia kuongezea uelewa maofisa hao kuhusu utunzaji misitu ya vijiji.

Chuwa alisema rasilimali mali misitu ikitunzwa kwa dhana ya uendelezaji itasaidia jamii kuinuka kiuchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!