Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi wamkataaa mwenyekiti wa kijiji kisa hekari 50
Habari Mchanganyiko

Wananchi wamkataaa mwenyekiti wa kijiji kisa hekari 50

Spread the love

WANANCHI wa kijiji cha Shinji kata ya Mbebe wilayani Ileje mkoani Songwe wamesema hawana imani na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ali  Kalinga kutokana na tuhuma za kuwamilikisha baadhi ya wananchi wakiwepo ndugu zake eneo lililotengwa na wananchi kwa ajili ya matumizi ya malisho ya mifugo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari 50. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endele).

Wakizungumza leo tarehe 28 Februari 2023 kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Kaimu afisa Tarafa ya Bulambya, Frank Mwampamba walisema mwenyekiti huyo alihusika kugawa maeneo hayo bila kushirikisha wajumbe wa halmashauri ya kijiji na wananchi waliopitisha kutenga eneo hilo tangu miaka ya nyuma.

Katika mkutano huo ambao Mwampamba alimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo, Farida Mgomi, mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Lingisoni Sikanyika alisema mwenyekiti huyo alitumia madaraka yake kuwagawia kwa nguvu baadhi ya ndugu zake na kushindwa kuwaondoa wananchi wengine waliovamia eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari 20.

Sikanyika alisema mwenyekiti  huyo awapishe kwani wameshindwa kuendelea kufanya naye kazi.

Amedai mwenyekiti huyo ameharibu matumizi bora ya mpango ardhi ya kijiji ambayo wananchi walikubaliana kupitia mkutano wa hadhara walitenga kwa ajili ya malisho na kuwagawia baadhi ya vijana wa kijiji hicho ambao watakuwa na uhitaji wa ardhi kwa ajili ya kulima na kujenga.

Naye Fikisoni Mwamlima (63) alisema tangu amezaliwa kijijini hapo wamekuwa na utamaduni wa kulinda maeneo hayo hivyo mwenyekiti ambaye walimchagua mwaka 2020 ameharibu utaratibu wa mpango wa matumizi ya ardhi.

Aidha, akijibu tuhuma hizo Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ali Kalinga alisema hahusiki na tuhuma hizo bali anatambua eneo hilo limevamiwa.

Licha ya kukiri baadhi maeneo waligawa na mtendaji bila kuwataarifu wananchi ameongeza kuwa alimuagiza mtendaji wa kijiji hicho kuwashughulika waliovamia eneo lililotengwa.

Diwani wa kata hiyo, John Katofani Mtafya alisema chuki ya wananchi kwa mwenyekiti huyo  imetokana na kugawa maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya kijiji bila kuwashirikisha wananchi ambao walitenga maeneo hayo ambayo walirithi kutoka kwa babu zao lakini leo wanashangaa maeneo kumilikiwa na watu.

Kaimu afisa Tarafa ya Bulambya, Frank Mwampamba alisema wanakijiji wanapaswa kuzisimamia Serikali zao za vijiji ili ardhi yao isichukuliwe bila kufuata utaratibu kwani kuna baadhi ya viongozi wasiokuwa waaminifu hugawa ardhi ya kijiji bila kuwashirikisha wenye ardhi yao.

Alisema asilimia 70 ya wakazi wa wilaya ya Ileje wanategemea kilimo na ufugaji kuendesha maisha yao ya kila siku, hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kupangilia na kutenga ardhi kulingana na mahitaji ya wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!