July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi walalamikia hospitali ya Mwananyamala

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mwananyamala, Sophinias Ngonyani

Spread the love

MGANGA Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mwananyamala, Sophinias Ngonyani leo amejibu tuhuma za wananchi wakazi wa maeneo hayo waliokuwa wakiilalamikia harufu mbaya inayotoka hospitalini humo. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, harufu hiyo mbaya imedumu kwa wiki mbili bila ya kupatiwa ufumbuzi wowote kwa kile kilichodaiwa kuwa ni harufu isiyo na madhara ambayo imetokana na uchafu uliotoka katika chumba cha upasuaji.

Baada ya Mwandishi wa gazeti hili kupata malalamiko toka kwa wananchi na kuchunguza kwa ukaribu chanzo cha harufu hiyo na kukosa uhakika wa jambo hilo, ndipo alipoamua kufunga safari hadi kwa mganga mkuu wa hospitali hiyo ili kupata ufumbuzi.

Dk. Ngonyani amekiri kuwepo kwa tatizo hilo hospitalini hapo, na kudai kuwa, harufu hiyo ilizuka baada ya shimo ambalo lilifukiwa takataka za kutoka chumba cha upasuaji kufukuliwa.

Amedai, kuna ujenzi wa vyumba maalum vya upasuaji kwa ajili ya wanawake tu ambao unaendelea katika maeneo hayo hivyo walilazimika kupitisha msingi wa vyumba hivyo maeneo hayo ya shimo.

“Kulikuwa na chumba kimoja tu cha upasuaji ambapo ililazimika wagonjwa wote wafanyiwe humo ambapo ilikuwa pia ni chanzo cha wagonjwa wengi kupewa rufaa ya kwenda hospitali nyingine kutokana na wingi wa wagonjwa,” amesema Ngonyani.

Ngonyani ameeleza kuwa, kadri siku zinvyozidi kwenda ndipo wagojwa wanaongezeka hivyo kupelekea kupokea hata wagonjwa 2,000 kwa siku na kusababisha mlundikano hospitalini hapo.

Mbali na wananchi wa maeneo hayo kuendelea kulalamika, Ngonyani amewataka kuendelea kuwa wavumilivu kwani ujenzi unaofanywa pale ni kwa faida yao kwani wao wenyewe ndio watakaotumia kwa ajili ya kujifungulia na kufanyiwa upasuaji.

Nakwamba, ujenzi huo unatarajiwa kumalizika ndani ya miezi sita ambapo Serikali kupitia manispaa ndio ambao wamedhamini ujenzi huo unaoendelea.

Kuhusu madhara ya ya harufu hiyo Dk Ngonyani amesema, “harufu hii haina madhara yoyote kwa binadamu kama inavyodaiwa, kwani kila siku tunaweka dawa ya kuuwa kemiko zote na kupunguza harufu hivyo tunatarajia hadi kufikia mwisho wa wiki hii itakuwa imeisha”.

error: Content is protected !!