July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi waivimbia serikali

Spread the love

WANANCHI wanaotumia usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam, wamepinga kauli ya serikali inayopiga marufuku abiria kusimama kwenye daladala ifikapo tarehe Mosi Januari, 2016. Anaandika Faki Sosi … (endelea)

Wakizungumza na MwanaHALISI Online watu hao wamesema kuwa, kauli hiyo ni ya utashi binafsi wa mawaziri wanaotaka kuonekana wachapakazi na haizingatii hali halisi.

Amani Godfrey ambaye ni dereva wa daladala la Gongo la Mboto kwenda Makumbusho amesema kuwa, iwapo serikali itasimamia kauli yake, waathirika wakubwa ni abiria wenyewe kutokana.

“Abiria ndio watakaoathirika zaidi kwa kuwa hakuna gari za kutosha na miundombinu hii haifai kwa kuwa inasababisha foleni kubwa,” amesema ambapo ameshauri serikali kuboresha miundombinu kwanza.

Dereva wa daladala inayofanya safari zake kutoka Mbagala kwenda Makumbusho, Issa Mshihiri amesema serikali ijiandae kuathirikakiuchumi kwa kuwa, abiria lazima wachelewe kazini kutokana na udhaifu wamiundombinu.

Mshihiri anasema kuwa pamoja na sasa abiria kusimama, bado wanateseka kupata usafiri “je, utaratibu huo ukitekelezwa si ndio balaa.”

Lakini pia amesema utaratibu huo utawanyima kipato kwa kuwa, anaweza kushindwa kufikisha kiwango anachohitaji tajiri kwa kuwa, fileni husababisha safari za kwenda na kurudi kuwa chache.

Salumu Issa ni kondakta wa daladala inayofanya safari zake kutoka Mbagala kwenda Makumbusho ambapo amesema kuwa, viongozi wengi serikalini hawajui shida za wananchi kutokana na kumiliki magari ya kifahari.

“Viongozi wetu hujianagilia utajiri wao na wanamiliki magari mengi hivyo wanadhani kila Mtanzania ana ukwasi kama wao, hawajui shida za usafi na wala hawakai kwenye foleni. Usishangae siku moja ukasikia kiongozi anapiga marufuku kuuza na kuvaa mitumba,” amesema.

Emmanuel Damian ambaye ni dereva wa gari litokalo Kariakoo kwenda Makumbusho amesema kuwa, hatua hiyo itawatia hasara wamiliki wa magari kutokana na kuwa miundombinu sio rafiki kwa mfumo huo unaotarajiwa kuanzishwa na serikali.

Mwalimu Mwenda ni miongoni mwa abiria wa Daladala ambaye anafanya biashara zake kwenye Soko la Makumbusho na mkazi wa Mbagala amesema kuwa, kauli hiyo haikufanyiwa utafiti kwani itapelekea watu wengi kupoteza ajira kwa kukosa usafiri wa kuenda kazini.

Shaziri Bakari ametupia lawama kwa viongozi kutokana na uamuzi huo bila ya kushirikisha wananchi.

error: Content is protected !!