Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wananchi wahimizwa kuwekeza kwenye hisa
Habari Mchanganyiko

Wananchi wahimizwa kuwekeza kwenye hisa

Mkurugenzi wa Bodi ya TCCIA, Donald Kamori
Spread the love

WANANACHI wametakiwa kuhudhuria semina zinahusua uwekezaji wa hisa ili wapate elimu itakayowasaidia kupata ufahamu kwa undani kuhusu biashara hiyo endelevu, anaandika Angel Willium.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya TCCIA Investment, Arphaxad Masumbu wakati wa kuanzimisha miaka 12 ya wanahisa nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Masumbu amesema wanachangamoto ya kutokuwa na watu wengi katika ununuaji wa hisa, hilo linatokana na wananchi kutokuwa na elimu juu ya biashara hiyo yan uwekezaji.

“Mikoani kumekuwa na mwitikio mdogo, wakushiriki semina za elimu kwa wananchi, hivyo tunaingia gharama kubwa kuandaa mikutano, watu hawajui kwamba biashara ya kununua na kuuza hisa ni endelevu kwani usipofaidika wewe basi itamsaidia mtoto wako,” amesema Masumbu.

Naye Mkurugenzi wa bodi ya TCCIA, Donald Kamori amesema wameimalisha mtaji wao ambao kwa sasa umefikia Tsh. 1.28 bilioni kutoka 1.9 bilioni, fedha hizo wamewekeza kwenye makapuni mbalimbali kama bank NMB na mengineyo.

TCCI Investment imeazimisha miaka 12 ya tangu kuanzishwa mwaka 2005, mwaka jana waliweza kutekeleza majukumu ya kusimamia zoezi la kuthaminisha mali za kampuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!