SERIKALI imeagiza wananchi kuendelea kufungiwa dira mpya za maji – Lipa Kadiri Utumiavyo – ili kupunguza malalamiko yao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hatua hiyo pia imeelezwa kuwa, itapunguza tatizo la malimbikizo ya madeni ya matumizi ya maji.
Jumaa Aweso, Naibu Waziri wa Maji ametoa kauli hiyo leo bungeni tarehe 2 Aprili 2019 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Jasmine Bunga.
Katika swali lake, mbunge huyo alisema, kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi dhidi ya mamlaka za maji katika halmashauri kwa kuwapatia wananchi bili kubwa za maji ambazo haziendani na uhalisia.
“Je, ni lini serikali itaanzisha utaratibu wa kulipa maji kadri utumiavyo, katika utoaji wa huduma za maji kama ilivyo kwenye umeme,”amehoji.
Aweso akijibu swali hilo amesema, serikali imeishaanza kutumia utaratibu wa kulipa maji kadri unavyotumia katika maeneo mbalimbali nchini.
“Kwa sasa utaratibu huo umeanza kutumika katika maeneo yanayohudumiwa na Mamlaka za Arusha, Iringa, Songea, Dodoma, Tanga, Mbeya, Tabora, Mwanza, Moshi na DAWASA,” amesema.
Leave a comment