July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi shirikianeni na asasi kuleta maendeleo-Kibamba

Spread the love

WANANCHI wametakiwa kuungana na tathimini zinazofanyika na asasi za kiraia katika kuimarisha maendeleo ya nchi kidemokrasia, uchumi na masuala utawala bora. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yamesemwa leo wakati wa mafunzo ya asasi mbalimbali za kiraia kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuhusu tathimini ya nchi za kiafrika za kuimarisha utawala bora chini ya Kituo cha utoaji wa Taarifa kwa wananchi Tanzania (TCIB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Fire kutoka chuo kikuuu cha Vitts nchini Afrika Kusini.

Mpango huo wa kwanza kushirikisha nchi za Afrika unaojulikana na kama Afrika Peal Review Mechanism (APRM) kuwezesha kujitathimini wenyewe badala ya kusubiri Ulaya na Marekani kufanya tathimini ya nchi za Afrika.

Mkurugenzi wa Kituo cha Taarifa kwa Wananchi (TCDB), Deus Kibamba amesema watanzania wanatakiwa kuunga mkono taasisi hizo kwa sababu ni mpango wa kidemokrasia unaolenga kujitathimini wenyewe badala ya kufanyiwa na nchi zilizopo nje ya Afrika.

Kibamba amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuelimisha wana asasi za kiraia kuweza kusaidia kusukuma maendeleo ya nchi kwa kufanya tathimini na kukusanya matatizo mbalimbali yanayoikumba nchi husika ili kuyawasilisha katika umoja wa Afrika ambao utamhoji Rais juu ya matatizo hayo.

Amesema kwa kupitia mpango huu, nchi za Afrika zitajitathimini zenyewe na kutatua matatizo yao badara ya kuwa na hofu kwa tathimini zinazotolewa na nchi za nje ya Afrika.

Akizungumzia sababu za kufanya mafunzo ya mpango huo ulioanzishwa tangu mwaka 2004, Kibamba amesema nchi 35 za Afrika zimejiunga tangu kaunzishwa kwa mpango huo lakini baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania zimekuwa nyuma katika ushiriki kutokana na baadhi ya asasi kutofahamu mpango huo unafanyaje kazi.

“Ndiyo maana tunafanya mafunzo haya kuwaelimisha waweze kuelewa ni jinsi gani zinatakiwa kushiriki katika mpango huu,” amesema Kibamba.

Amesema pia nchi nyingi za Afrika hazipendi kujitathimini wenyewe hali inayopelekea kusubiri kutathiminiwa na nchi nyingine kama Marekani juu ya mwenedo wao wa kimaendeleo wakati wanao uwezo wa kuyafanya hayo wenyewe.

error: Content is protected !!