January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi Nyamagana waibana Tanesco

Spread the love

WANANCHI wa Kata na Kijiji cha Kishiri Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza juzi waliwabana viongozi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kutokana na mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) awamu ya pili kumalizika huku baadhi yao wakiwa hawajaunganishwa na umeme. Anaandika Moses Mseti … (endelea).

Viongozi hao wa Tanesco ni Meneja wa Kanda ya Ziwa, Amos Maganga; Kaimu Meneja wa Mkoa wa Mwanza, Gerson Manase; Kaimu Meneja wa Wilaya ya Nyakato, King Fokanya; Mhandisi wa Mradi wa REA Mkoa wa Mwanza, Leon Matata na Ofisa Uhusiano, Flavian Moshi.

Hata hivyo, viongozi hao walifika kwenye Kata ya Kishiri kwa ajili ya kupokea kero za wananchi hao baada ya wakazi 500 kupata umeme huku wengine zaidi 4,000 wakikosa huduma ambapo ilidaiwa kufanyika kwa vitendo vya rushwa, kitendo kilichosababisha kuwapo malalamiko mengi na kumfikia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.

Wananchi hao walitaka kujua sababu ya wananchi wachache kupata umeme wakati kuna idadi kubwa ya wakazi kukosa, pia walitaka kujua kitendo cha viongozi wa kisiasa kujihusisha na mradi huo na kuchukua rushwa ili kupata umeme, baadhi ya nyumba kutounganishiwa umeme licha ya nguzo kuwa karibu na wengine walitaka kujua ni lini mitaa ya Kanindo, Ihushi, Bukaga, Fumagila, Kilimo na Bushitu.

Wananchi waliwashambulia kwa maneno makali baada ya viongozi hao kuwaeleza kuwa wakazi 500 waliounganishiwa umeme ndio walikuwa walengwa kutokana na tathmini iliyofanyika mwaka 2011 kabla ya kuwapo na ongezeko la wananchi ambao nao walistahili kupewa huduma hiyo.

Pia viongozi hao waliwaeleza wananchi kwamba, mitaa iliyokosa umeme awamu ya pili, wataupata awamu ya tatu baada ya Serikali kukaa na kufanya tathmini nyingine, kitendo kilichosababisha wananchi kulalamika huku wengine wakirusha maneno makali.

Baadhi ya wananchi waliochangia ni pamoja na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilimo, Deusdict Malinyi; Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa wa Kishiri B, Mashaka Masami; Jeremia Lujongo, Augostino Libalema; Maximilian Augostino, Gabriel Mgaya; Elizabert John, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kanindo, Hongolo Kachongwa na wengine wengi.

Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Maganga alifanya kazi ngumu ya kuwaelemisha wananchi ambapo alikiri kwamba Kishiri haikutakiwa kupewa umeme wa REA kwa sababu ipo mjini na ina miradi mikubwa ambayo umeme huo hauwezi kuendesha baadhi ya mashine kwa kutumia nyaya zenye njia mbili (phase II).

“Kazi ya Tanesco ni kutafuta wateja, nakiri Kishiri mnahitaji umeme lakini kwa bahati mbaya mradi huu umetekelezwa kwa tathmini ya awali iliyoonyesha watu 500 wanahitaji kutapata umeme, sasa tunaomba malalamiko yenu tumeyachukua ili kwenda kukaa kuona ni namna gani ya kuwapatia huduma hii muhimu.

“Nasikitika sana kusikia mlitozwa fedha kupata umeme, kitendo cha wanasiasa kuingilia masuala ya tanesco ni kudandia jambo lisilowahusu, nasema walifanya kosa, haiwezekani mkatozwa 50,000 hadi 250,000 ili kupata nguzo na masuala mengine, ila nawahakikishia kwamba wale walio karibu na nguzo watapata umeme kati ya mwezi huu hadi Januari, 2016 kwa gharama ya Sh 27,000 tu.

“Lazima tukiri Tanesco ipo nyuma katika kuwahudumia wananchi, tatizo ni bajeti inayotolewa na serikali, ila tunakwenda kuangalia ni wapi mradi unasuasua wa REA ili tuuhamshie hapa Kishiri,”amesema huku Kaimu Meneja mkoa huo, Manase akiongeza kuwa tayari wamepata ridhaa ya kuwaunganishia wakazi wengine 273 wa Kishiri ambao wamepitia na nguzo karibu.

 

error: Content is protected !!