Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi Mvomelo walia kuporwa ardhi
Habari Mchanganyiko

Wananchi Mvomelo walia kuporwa ardhi

Spread the love

WANANCHI wa vijiji vya Kunke na Mlumbilo, Mvomero mkoani Morogoro wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi uliopo baina yao na Uongozi wa Msitu wa Hifadhi wa TFS unaowataka kupisha eneo wanaloishi linalodaiwa limo ndani ya msitu wa Pagale bila kujali maslahi yao kama wananchi waliokaa muda mrefu kwenye eneo hilo, anaandika Christina Haule.

Hassan Suleiman mkazi wa Kitongoji cha Mafleta B –Pagale kijiji cha Kunke amesema mbele ya Diwani wa Kata ya Mtibwa, Lucas Mwakambaya, anashangazwa kuona watu wanakuja kupima maeneo ya yao bila ridhaa yao ama kuitishwa mkutano wowote wa kijiji.

Amesema upimaji huo haukuwa uliofuata kanuni kwani wapimaji walidai kuwa wanafanya hivyo kutekeleza agizo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Mwalimu Mohamed Utaly la kuwataka kuhama ifikapo Agosti 30 mwaka huu kwa kile kinachodaiwa kuwa wamevamia msitu wa hifadhi.

Aidha amesema kuwa licha ya kuwa walisambaza waraka huo ukiwataka wananchi wajiandae kuhama kwa madai kuwa wamevamia msitu huo wa hifadhi wa Pagale kwa madai kuwa wanataka kufanya uoteshaji wa zao la mitiki lakini na wao kama wakazi wa miaka mingi kwenye eneo hilo walipaswa kusikilizwa na sio kupewa notisi ya kuhama pekee.

“Sisi tumekaa hapa kwa muda mrefu kabla ya msitu wa hifadhi kuwekewa mipaka mwaka 1952 na wakoloni hivyo tunashangaa kuambiwa tuhame bila ya kuitishwa mkutano wowote kuelezwa rasmi na pia tulipwe ili kuweza kuanzisha makazi mapya,” anasema Suleiman.

Hivyo walimuomba Rais Dk. John Magufuli kuwasaidia kubakia katika maeneo yao kufuatiwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya kutoa tamko hilo ambalo kwao bado lina utata.

Naye Enedius Mpesa mkazi wa kitongoji cha Masangarawe kijiji cha Mlumbilo, amesema wamekuwa wakiishi katika kijiji hicho na kufanya shughuli za kilimo na kuishi na hivyo kutekeleza agizo la Rais JPM la kulima badala ya kuitegemea serikali kuwapa msaada hivyo wanaoimba serikali endapo watahamishwa watengewe eneo jingine la makazi na kufanya shughuli za kilimo kwani hawana pa kwenda.

Meneja Hifadhi ya Misitu Wilaya ya Mvomero (TFS), Husna Msagati alipoulizwa kuhusu sakata hilo aliwaondoa hofu wananchi hao kuwa wao hawana lengo la kumfukuza mwananchi bali wanatekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kuhakikisha maeneo ya hifadhi za misitu yanapimwa na kuwekewa maboya (Becons) ili kuepusha wananchi wanaovamia, kufanya makazi, ama shughuli za kibinadamu ikiwemo kuvuna mbao katika misitu bila ya kufuata sheria.

“Tunatekeleza agizo la waziri mkuu, hatuna haja ya kuwahamisha wananchi na endapo itabidi kuwaondoa itabidi tukae na uongozi wa mkoa ili kujadili kwa pamoja na hapa busara lazima itatumika bila ya kuwaathiri wananchi,” amesema.

Katibu tawala wa Wilaya ya Mvomero, Michael Maganga akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya kuhusu tamko hilo amesema kuwa hawezi kulizungumzia mpaka mkuu wa wilaya huyo atakaporudi toka safarini na kusema kuwa wananchi wa vijiji hivyo wamepewa muda wa kuhama ili kuweza kuvuna mazao yao mashambani huku taratibu nyingine zikifanyika.

Awali Diwani wa Kata ya Mtibwa, Lucas Mwakambaya aliwataka wananchi hao kutokuwa na hofu kufuatia kuishi mahali hapo kisheria kama kijiji tangu kijiji iliposajiliwa mwaka 1999 ambapo alimuomba Rais Magufuli kuunda tume ya kuchunguza mgogoro huo ili wananchi hao waweze kupata haki yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!