Saturday , 4 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wananchi kuamua hatma mapendekezo ya UN yaliyowekwa kiporo na Serikali
Habari Mchanganyiko

Wananchi kuamua hatma mapendekezo ya UN yaliyowekwa kiporo na Serikali

Spread the love

MAPENDEKEZO 65 ya uimarishaji haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (UN), ambayo Serikali ya Tanzania ilikataa kuyatekeleza kwa sababu mbalimbali, yatafikishwa kwa wananchi ili waamue kama yakubaliwe au la. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamelezwa leo Alhamisi, tarehe 12 Mei 2022 na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro, akifungua kikao kazi cha kupitisha mpango mkakati wa Asasi za Kirai.

Kuhusu utekelezaji wa mapendekezo 167 kati ya 252, yaliyokubaliwa na Tanzania kwenye duru la tatu la Mchakato wa Tathimini ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UPR).

Waziri huyo wa Katiba na Sheria amesema, Serikali ilikataa kuyapokea mapendekezo hayo kwa kuwa yalikuwa yanakinzana na misingi ya katiba, sheria, tamaduni na mila za Kitanzania, hivyo itatoa nafasi kwa wananchi kuyajadili kama yanafaa kupitishwa.

Dk. Ndumbaro amesema, kama wananchi watayaafiki mapendekezo yote au baadhi ambayo hayakinzani na mila na desturi za nchi, Serikali itarekebisha sheria husika ili yafanyiwe kazi.

“Baadhi ya mapendekezo haya 65 yalikuwa yanakinzana na katiba na mapendekezo mengine yalikuwa yanapingana na sera, sheria, mila na tamaduni za Watanzania au Afrika, katika haya mapendekezo hatujafunga mjadala tunaendelea kujadili ili Watanzania waseme kama mapendekezo hayo yanakinzana na katiba yetu tubadilishe au tuyaache,” amesema Dk. Ndumbaro.

Waziri huyo amesema “Watanzania wakishasema hayo sisi kwetu inabaki ni kutekeleza. Nasema hili kusisitiza kwamba sisi ni wawakilishi hivyo ni vizuri tutege masikio kwa wananchi wetu ambao tunawawakilisha tujue wanataka nini na hawataki nini.”

Dk. Ndumbaro amesema kama Watanzania watayakubali baadhi ya mapendekezo hayo, Serikali itapeleka bungeni muswaba wa sheria husika ili zifanyiwe marekebisho yatakayowezesha utekelezaji wake.

Kwa mara ya kwanza Serikali ilipokea mapendekezo 108 kati ya 252, lakini baadae iliongeza mapendekezo hayo hadi kufikia 167.

Miongoni mwa mapendekezo ambayo Serikali ilikataa kuyapokea ni yanayotetea haki za mapenzi ya jinsia moja na ufutwaji wa adhabu ya kifo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!