August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wanamtandao’ wa ujangili kizimbani

Spread the love

WATU 10 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa kuratibu mtandoa wa ujangili unaojihusisha na usafirishaji wa meno ya tembo, anaandika Faki Sosi.

Watuhumiwa hao ni pamoja Ally Sharif (28), aliyekuwa akiishi Tabata Segerea, Raia wa Gunea; Victory Mawalla (29) Mkazi wa Kimara; Calist Mawalla (22) Mkazi wa Kibamba; Haruna Kassa (37) Mkazi wa  Mwanangati.

Wengine ni Abbasi Jabu (40); Mkazi wa Mwanangati;  Solomon Mtenya (46), Mkazi wa Kimara; Mussa Ligagabile, Mkazi wa Mbagala; Fatoumata Saumaolo (34) aliyekuwa akiishi Tabata Segerea, pia Raia wa Gunea; Khalfan Kahengele, Mkazi wa Keko na Ismail Kassa, Mkazi wa Kipunguni ‘B’.

Akiwasoma mashtaka hayo Paul Kadushi mbele Yohona Yongola Hakimu Katika Mahakama hiyo amedai kuwa,  watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa makosa matatu pamoja na  kuhusika katika mtandao wa uharifu.

Kadushi amedai kuwa,  kati ya tarehe 6 Aprili na 23 Machi mwaka huu watuhumiwa hao walipanga na kuratibu ununuzi na usafirishaji wa nyara za serikali ambazo ni  meno 660 yenye thamani ya Sh.4.5 bilioni.

Shitaka la pili ni kujihusisha na usafirishaji wa nyara za serikali bila ya kibali cha maofisa wa wanyama pori ambapo walitenda hayo  tarehe 6 Aprili na 23 Machi mwaka huu.

Wakati kesi hiyo ikiendelea

Shitaka la tatu linawahusu watuhumiwa watano pekee ambao ni Ally Sharif, Victory Mawalla, Calist Mawalla, Haruna Kassa, Abbasi Jabu ambao wanatuhumiwa kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali ambazo meno ya tembo 660 yenye thamani ya Sh.4.5 bilioni.

Hakimu Yongola amesema kuwa, mahakam  haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo  na kwamba, watuhumiwa hao wahakuweza kujibu shauri hilo

Upelelezi huo haujakamilika hivyo shauri hilo litatajwa tena  tarehe 28 Julai mwaka huu watuhumiwa  wote wamerudishwa lumande .

 

error: Content is protected !!