May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanamichezo Urusi, Belarus wapigwa marufuku Paralimpiki

Spread the love

WANAMICHEZO wote waliotarajia kushiriki michezo ya Paralimpiki msimu wa baridi, inayotarajiwa kuanza rasmi kesho Beijing nchini China, wamepigwa marufuku. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Kimataifa ya Paralimpiki (IPC) leo tarehe 3 Machi, 2022, imesema hali ni mbaya katika kijiji inakofanyika michezo hiyo na imekuwa vigumu kuhakikisha usalama wa wanamichezo hao unaendelea kuwepo.

Uamuzi wa awali wa IPC kuruhusu wanamichezo 71 wa Urusi na 12 wa Belarus kushiriki bila kuonyesha upande wowote, umekosolewa vikali.

“Tunaamini kabisa kuwa michezo na masuala ya kisiasa hayapaswi kabisa kuchanganywa,” amesema Rais wa IPC katika taarifa yake hii leo na kuongeza;

“Hata hivyo, ni bahati mbaya kwamba vita vimeingia katika hii michezo na nyuma ya pazia Serikali zimekuwa na ushawishi katika tukio letu.”

error: Content is protected !!