July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanamichezo 10 wenye mkwanja mrefu duniani

Bondia Floyd Mayweather akionesha jeuri ya fedha

Spread the love

IMEDHIHIRISHA Floyd Mayweather Jr. ‘May Money’, hajapewa jina hilo kwa makosa. Anaandika Benedict Kimbache … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na jarida la Forbes kwa mwaka 2015 juu ya wanamichezo 100 waliolipwa fedha nyingi zaidi duniani, taarifa iliyotolewa siku ya Jumatato wiki hii, Mayweather ameibuka mshindi wa kwanza, na amekuwa akishikilia nafasi hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo.

Fedha alizolipwa ni zaidi ya fedha zilizolipwa kwa wanariadha watatu waliopo chini yake zikijumlishwa kwa pamoja, akiwazidi kwa dola milioni 13.

Mayweather, ametengeneza dola milioni 200 ( bilioni 400), zaidi ya fedha za kashfa ya Escrow. Fedha hizi zilitokana na malipo kwenye pambano lake na Manny Pacquiao, pambano lililoingiza jumla ya dola za marekani milioni 600.

Manny Pacquiao amekuwa wa pili hata hivyo mwaka 2014 alikuwa mtu wa 11. Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Roger Federer wameshika nafasi za tatu, nne na tano.

Hii inamaanisha hakuna hata mwanariadha mmoja kutoka Marekani kutoka kwenye fani za mpira wa mguu, mpira wa kikapu na mpira wa besiboli ameshika nafasi katika tano bora.

Kwa mwaka wa sita mfululizo mchezaji mahiri wa mpira wa Tenisi Maria Sharapova (dola milioni 29.7) amekuwa mwanamke aliyelipwa kiwango kikubwa.

Hapa ni orodha ya wanamichezo 20 waliolipwa kiwango kikubwa:

  1. Floyd Mayweather Jr.(ngumi): $300 milioni
  2. Manny Pacquiao (ngumi): $160 milioni
  3. Cristiano Ronaldo (mpira wa miguu): $79.6 milioni
  4. Lionel Messi (mpira wa miguu): $73.8 milioni
  5. Roger Federer (tenisi): $67 milioni
  6. LeBron James (mpira wa kikapu): $64.8 milioni
  7. Kevin Durant (mpira wa kikapu): $54.1 milioni
  8. Phil Mickelson (gofu): $50.8 milioni
  9. Tiger Woods (gofu): $50.6 milioni
  10. Kobe Bryant (mpira wa kikapu): $49.5 milioni

Orodha zaidi soma hapa 

error: Content is protected !!