June 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanakijiji wajipanga kumng’oa mwenyekiti wao

Spread the love

WANANCHI wa Kijiji cha Kisemvule wilayani Mkuranga, Pwani wamepanga kumng’oa Omar Makunga, mwenyekiti wa kijiji hicho kwa madai ya kutokuwa muadilifu pia kufanya uamuzi bila kushirkikisha wanakijiji, anaandika Faki Sosi.

Mwandishi wa mtandao huu amefika kijijini hapo jana na kukutana na wananchi ambao wameeleza kuwa, wanapanga kumng’oa mwenyekiti wao kutokana na tuhuma hizo ikiwemo kuhujumu mapato ya kijiji hicho.

Bakonda Fupi, Mwanakijiji wa Kisemvule amesema kuwa, sababu za kumng’oa kiongozi huyo aliyeongoza kwa miaka 20 pia ni kutokana na kuwa na tabia ya kutowasomea wananchi mapato na mwenendo wa miradi ya kijiji.

Fupi amedai kuwa, kiongozi huyo anahusika na migogoro ya ardhi inayotokea kijijini hapo kutokana na kuuza kiwanja kimoja mara mbili

Amesema kuwa, mwenyekiti wa kijiji hicho haaminiki na wananchi kutokana na kutoa stakabadhi bandia za mauzo ya viwanja ambapo pesa zinazopatikana kwenye uuzaji huo haziingizi kwenye mapato ya kijiji.

Rajabu Chopa, Mwanakijiji wa Kijiji Kisemvule amesema kuwa, mwenyekiti wa kujiji hicho hukeuka makubaliano waliyoafikiana na wanakijiji kwenye mikutano ya uamuzi wa kijiji hicho.

Chopa amedai kuwa, mwenyekiti huingia mikataba na viwanda bila ya wanakijiji kujua wala kuwaambia ambapo hushangazaa kuona ugeni wa kiwanda bila kujua kimefikaje kwenye kijiji chao.

“Mwenyekiti akishirikiana na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kisamvule wamekiuka amri ya Rais ya elimu bure kwa kuwatoza kiasi cha shilingi 40,000 kwa wazazi wanafunzi wa shule hiyo ambapo sisi wananchi tulitaka kurudishiwa fedha lakini mwenyekiti huyo ameweka mkwamo,” amesema Chopa.

Alipotafutwa mwenyekiti huo (Omar) kuelezea tuhuma hizo kutoka kwa wananchi wa eneo lake, alijibu kwamba “nipo buy na vikao.”

Kabla ya kutamka kauli hiyo, mwandishi alizungumza naye kwa simu na kujitambulisha lakini alipoelezwa tuhuma zake, ndipo alipotoa kauli hiyo.

error: Content is protected !!