Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wanakijiji waapa kumchagua diwani aliyeanza kutatua kero
Habari za Siasa

Wanakijiji waapa kumchagua diwani aliyeanza kutatua kero

Spread the love

WANAKIJIJI wa kijiji cha Mkono wa Mara kata ya Mkambarani, Morogoro wamesema watamchagua mgombea udiwani wa kata hiyo Charles Mboma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa atawaletea maendeleo waliyakosa toka mwaka 1964 kijiji kilipoanzishwa. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Wakizungumza na waandishi wa habari jana kijijini hapo, wanakijiji hao walisema kuwa kijiji hicho kimesahaulika tangu mwaka 1964 kilipoanzishwa kwenye mpango wa oparesheni vijiji na hivyo kupelekea kukosa huduma muhimu kama umeme, maji, zahanati pamoja na miundombinu.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM tawi la Mwanika, Anthony Kunambi alisema kijiji hicho kimesahaulika toka enzi za oparesheni vijiji hali iliyopelekea wakazi wake kuishi maisha ya tabu na mahangaiko.

‘’Cha ajabu toka mwaka 1964 mpaka leo hatukumbukwi, hakuna barabara, maji, umeme wala zahanati, kijiji hiki kiko umbali wa km 28 toka Mkambarani senta, tunahitaji umeme, barabara, maji na zahanati, tuna imani sana na Diwani wetu mteule kuwa atalisimamia hili sababu ameweza kusaidia ujenzi wa matundu 8 ya vyoo katika shule ya msingi mkambarani wakati akiwa hana Hata wazo la kugombea’’ alisema Kunambi.

Nae Mjumbe wa Halmashauri ya kata ya Mkambarani Japhet Mpenda, ambae pia ni mkazi wa kijiji hicho alisema kijiji hicho kipo nyuma kimaendeleo ikiwemo suala la elimu na afya hali inayopelekea akina mama wajawazito na watoto kuhangaika kwa kukosa kituo cha kupimia afya zao na watoto wao na kulazimika kutembea umbali Wa kilometa 15 kwenda kwenye Zahanati ya jeshi mkono Wa Mara kupata matibabu.

‘’Hakuna zahanati, huwa tunajitahidi kutafuta waganga ili kuwapima watoto na kujua wanavyoendelea, watoto huninginizwa juu ya mti, tiba tunapata Taasisi ya magereza, ila kuna umbali sana kufika huko na gharama ni kubwa, kwa pikipiki ni shilingi elfu kumi na tano, wengine wanashindwa kabisa hususani wajawazito wakitaka kujifungua, tumefurahi kwa kupata diwani mteule, tuna imani nae sana atatusaidia’’ alisema.

Kwa upande wake mgombea udiwani Wa kata hiyo ambaye hana mpinzani Charles Mboma, alisema changamoto hizo pamoja na zingine zinazowakabili wananchi wa kata hiyo, ndizo zilizomsukuma kuwania nafasi hiyo ili aweze kutoa mchango wake kwa kushirikiana na wananchi ili kuleta maendeleo.

‘’Kilichonivutia ni kutoa mchango wangu katika kata yangu na Halmashauri ya Wilaya ya  Morogoro, pia kutokana na kuona baadhi ya maeneo mambo hayaendi vizuri, ikiwemo sekta ya elimu, tuna matatizo ya madarasa, shule nyingi kuchakaa, vyoo na upungufu wa sekondari, na wananchi wetu wanaishi maisha ya umasikini sana’’ alisema Diwani hiyo mteule.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!