Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanajeshi 8 wahukumiwa kifo kwa mauaji ya Mchina
Kimataifa

Wanajeshi 8 wahukumiwa kifo kwa mauaji ya Mchina

Kitanzi
Spread the love

 

WANAJESHI nane na raia moja katika eneo la kaskazini mashariki mwa DRC lililogubikwa na vita, wamehukumiwa kifo kwa mauaji raia mmoja wa China na ubadhirifu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Wote walipatikana na hatia ya mauaji na kujihusisha na uhalifu wakiwemo kanali Mukalenga Tendeko na Kayumba Sumahili.

Wanajeshi wengine watatu ambao walikuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela katika kesi hiyo, waliachiliwa huru.

Maafisa hao wawili wakuu walituhumiwa kupanga shambulio dhidi ya msafara uliokuwa umebeba dhahabu, pesa taslimu dola 6,000 na wafanyakazi raia wa China kupitia eneo la Irumu katika jimbo la Ituri nchini humo.

Msafara huo ambao ulikuwa unarejea kutoka mgodi wa dhahabu, ulishambuliwa tarehe 17 Machi mwaka huu kwenye kijiji cha Nderemi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!