TAKRIBAN wanajeshi 70 wameuawa katika shambulio la mizinga lililofanywa na wanajeshi wa Urusi katik miji muhimu ya Ukraine. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 1 Machi, 2022 na mofisa wa Ukraine imesema wafanyakazi wa dharura wanajaribu kutafuta majeruhi katika Kituo cha kikanda cha Kherson ambacho sasa kimezingirwa na wanajeshi wa Urusi.
Hayo yanajiri wakati wanajeshi wa Urusi wakidaiwa kumiminika vifaa zaidi vya kivita na kuuzingira Mji Mkuu wa Ukraine –Kyiv.
Jeshi hilo la Urusi linaidaiwa kusonga mbele kwa kasi huko Kyiv, na picha za satelaiti zinazoonyesha msafara wa vifaa hivyo vya kivita ambao una urefu wa maili 40 sawa na Kilomita 65.
Makumi ya raia waliuawa mapema jana Jumatatu katika shambulio la makombora la Urusi kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kharkiv.
Leave a comment