March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanaharakati wazidi kumsakama mke wa Mugabe

Mwanamitindo Gabriella Engels aliyeshambuliwa na Grace Mugabe

Spread the love

GABRIELLA Engels, mwanamitindo nchini Afrika Kusini aliyeshambuliwa na Grace Mugabe, mke wa Rais wa Zimbabwe, amepinga kinga ya kidiplomasia inayotolewa na serikali ya nchi yake kwa vigogo, anaandika Irene Emmanuel.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 20 anaungwa mkono na kundi la shinikizo, AfriForum, ambalo katika kupinga sheria hiyo wameonyesha ukurasa wa kwanza wa fomu ya maombi kutoka mahakama kuu ya mji mkuu na kudai kwamba waziri wa mambo ya nje, Maite Nkoana Mashabane ameelezea sheria ya kinga ya kidiplomasia vibaya.

AfriForum wamedai kuwa sheria hiyo ya kidiplomasi inayowakinga vigogo na serikali haihusishi vigogo ambao wamesababisha vifo au majeraha kwa wananchi wake.

Polisi wa Afrika Kusini wamesema Grace hajaripoti kituoni kama ambavyo ilikuwa imepangwa na ameondoka nchini na mume wake Robert Mugabe jumapili iliyopita.

error: Content is protected !!