Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wanaharakati washtushwa gazeti la Uhuru kufungwa
Habari Mchanganyiko

Wanaharakati washtushwa gazeti la Uhuru kufungwa

Onesmo Olengurumwa
Spread the love

 

WANAHARAKATI nchini Tanzania, wameshtushwa na hatua ya Serikali kulifungia kwa muda wa siku 14, Gazeti la Uhuru linalomilikiwa na Chama Tawala nchini humo, cha Mapinduzi (CCM), kwa kosa la kumlisha maneno Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Gazeti hilo lilifungiwa jana tarehe 11 Agosti 2021, baada ya kuchapisha habari yenye kichwa ‘Sina wazo la kuwania urais-2025-Samia’, inayodaiwa kuwa ya uongo dhidi ya Rais Samia, kinyume na Sheria ya Huduma za Habari ya 2006.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kupitia Mratibu wake, Onesmo Olengurumwa, umepinga hatua hiyo kwa maelezo kwamba, Serikali imetoa adhabu pasina kuwapa nafasi ya kujitetea wahusika.

“THRDC imesikitishwa na uamuzi wa Serikali kusitisha leseni ya Gezeti la Uhuru kwa siku 14, kuanzia kesho (leo), ambayo inalifanya gazeti hilo kusitisha shughuli zake,” imesema taarifa ya Olengurumwa.

Mtandao huo, umesema ni vyema hatua zingechukuliwa kwa mwandishi wa habari aliyeandika habari hiyo, badala ya kulifungia gazeti, huku ikilitaka gazeti hilo likate rufaa kupinga uamuzi huo.

“Kufuatia kusitishiwa leseni, Uhuru lina haki ya kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana ya habari ndani ya siku 30. Tunadhani ingekuwa vyema kuchukua hatua dhidi ya mwandishi na sio kusitisha shughuli zake,” imesema taarifa ya THRDC.

THRDC, imeiomba Serikali ifanyie kazi hukumu ya Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ), inayoielekeza ibadilishe vifungu kandamizi vya Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, vinavyominya uhuru wa vyombo vya habari kujieleza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Anna henga, akizungumza na MwanaHALISI Online, leo tarehe 12 Agosti 2021, amesema hatua ya Serikali na CCM kulifungia gazeti lake inashangaza.
Huku akitoa wito kwa wahuiska kupewa nafasi ya kujitetea.

“Hatua hii ina changamoto, nimeshangaa safari hii wanajifungia wao kwa wao, ingawa hatua hii imeleta mizania juu ya hatua zilizochukuliwa katika magazeti mengine, ila cha muhimu wangewapa nafasi ya kujieleza,” amesema Henga na kuongeza:

“Walikuwa wanapaswa kujieleza, tunasema mtu apewe nafasi ya kujieleza, ku-proove (thibitisha) kwamba nilifanya uchunguzi nili-balance stori. Kama inaonekana ina makosa lifungiwe. Lakini uamuzi huo ulikuwa wa haraka sana, sidhani kama walipata nafasi ya kujitetea.”

Kabla ya Serikali kulifungia gazeti hilo, CCM kilitangaza kulifunga kwa muda wa siku saba kuanzia leo, huku chama hicho kikiwasimamisha kazi viongozi wa Uhuru, ili kupisha uchunguzi.

Viongozi wa Uhuru waliosimamishwa ni, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Media Group, inayochapisha gazeti hilo, Ernest Sungura. Mhariri Mtendaji, Athumani Mbutuku na Msiammizi wa gazeti hilo, Rashid Zahoro.

CCM ilichukua hatua hiyo saa kadhaa baada ya gazeti lenye habari hiyo kusambazwa mitaani na kuzua mjadala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!