August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanaharakati wanne wanyongwa na jeshi la Myanmar

Spread the love

 

SERIKALI ya kijeshi nchini Myanmar, imewaua wanaharakati wanne wa demokrasia nchini humo, ambao ilikuwa ikiwatuhumu kusaidia katika kutekeleza kile walichokiita, “matendo ya kigaidi.” Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo ya utawala wa kijeshi, imelaumiwa vikali na mataifa mengi ulimwenguni.

Wakihukumiwa kifo katika kesi za faragha iliyofanyika Januari na Aprili, mwaka huu, ni Kyaw Min Yu (53), almaarufu Jimmy, Phyo Zeya Thaw, ambaye aliyekuwa mwanasheria na msanii; Hla Myo Aung na Aung Thura Zaw.

Wanaume hao walishutumiwa kwa kusaidia vuguvugu la upinzani kupambana na jeshi lililotwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka jana na kuanzisha msako wa umwagaji damu dhidi ya wapinzani wake.

Gazeti la the Global New Light of Myanmar limeripoti kuwa Kyaw Min Yu na Phyo Zeya Thaw, walikuwa marafiki wa muda mrefu wa kiongozi aliyeondolewa madarakani, Aung San Suu Kyi.

Walidaiwa kushindwa katika rufaa dhidi ya hukumu zao za mwezi Juni.

Erwin Van Der Borght, mkurugenzi wa kanda wa shirika la haki la Amnesty International amesema, mauaji hayo ni sawa na mauaji ya kiholela; na ni mifano mingine ya rekodi ya ukandamizaji wa haki za binadamu ya Myanmar.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Myanmar (NUG), iliyopigwa marufuku na uongozi wa kijeshi nchini humo, imetoa wito wa hatua za kimataifa dhidi ya jeshi hilo.

Shirika la reuters limeripoti kuwa msemaji wa ofisi ya NUG, Kyaw Zaw, amesema kuwa jamii ya kimataifa lazima iuadhibu utawala huo wa kijeshi kwa ukatili wake.

Huku hayo yakijiri, Ufaransa imelaani mauaji hayo na kuyataja kuwa kupindukia kwa ukandamizaji wa utawala wa kijeshi wa nchi hiyo.

Taarifa kutoa kwa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa, imesema kuwa ijapokuwa hakuna mauaji yaliofanyika katika taifa hilo kwa zaidi ya miaka 30, mauaji ya aina hii yanachangia kupindukia kwa ukandamizaji wa utawala wa kijeshi na awamu nyingine katika kuongezeka kwa ukatili uliofanywa na utawala wa jeshi la Burma tangu mapinduzi ya kijeshi.

Wakati huo huo, Marekani pia imelaani mauaji hayo na kutoa wito kwa utawala wa nchi hiyo kuacha ghasia mara moja na kuwaachia huru wale waliozuiwa kinyume cha sheria.

error: Content is protected !!