March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanaharakati wainuka na kupaza sauti

Mkuregenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Hellen Kijo -Bisimba

Spread the love

KITUO cha  Sheria Haki za Binaadamu Nchini (LHRC), kimesema kwa sasa hali ya usalama hapa nchini ni siyo nzuri baada ya kuwapo matukio ya mashambulizi a silaha za moto, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuregenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Hellen Kijo -Bisimba amesema tukio la hivi karibuni la kupigwa risasi  Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Tundu Lissu ni ishara mbaya katika masuala ya usalama.

Aidha, amesema kuwa mashambulizi mengine ni yake yaliyofanywa kwa kampuni ya mawakili ya  IMMMA ya jijini Dar es Salaam na kuharibu mali mbalimbali.

Mwanaharakati huyo amesema shambulio la kupigwa Lissu kwa Risasi limewastua na na kulilaani tukio hilo kwenye nchi.
Amesema kuwa shambulio la Lissu limetishia sana watetezi wa haki za binaadamu kutokana na Lissu kuwa mtetezi wa masuala mbalimbali hapa nchini.

Dk.Bisimba amesema  kuwa hivi Karibu kumetokea vitendo vya kutekwa kwa wananchi ndani ya nchi yao kufariki kwa Raia na Askari Kibiti Pwani .

Tukio lingine alilotaja la kuashiria uvunjifu wa amani ni tukio la hivi karibuni la kumtishia bastola, Nape Mnauye Mbunge na Mtama (CCM).
Ameshauri serikali kutafuta msaada kwa ajili ya kufanya upelelezi wa kina ili kukomesha vitendo hivi vya uhalifu.

error: Content is protected !!