May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanaharakati wahukumiwa kifungo cha maisha nchini Misri

Moja ya maandamano ya wanaharakati wa Ikhwanul Muslimin

Spread the love

Mahakama ya Jinai nchini Misri imewahukumu kifungo cha maisha jela wanaharakati 43 wa Ikhwanul Muslimin, anaandika Hellen Sisya.

Katika hukumu hiyo mahakama hiyo imesema wanaharakati hao walishiriki maandamano yaliyopigwa marufuku dhidi ya serikali, kuwashambulia maofisa usalama na kupora mali za umma.

Aidha, mahakama hiyo pia imewaamuru watunhao kulipa faini ya Dola za Marekani  948,661 kwa kupora mali za umma.

Wanaharakati wengine tisa wa Ikhwani wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela huku 92 wakiachiwa huru.

Baada ya jeshi la Misri kumuondoa madarakani Muhammad Mursi serikali ilipiga marufuku shughuli zote za kundi hilo la  Ikhwanul Muslimin.

Kadhalika, idadi kubwa ya viongozi na wanachama wa kundi hilo wamefungwa jela na baadhi yao wamehukumiwa adhabu ya kifo.

error: Content is protected !!