Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanahabari watakiwa kuweka kando taarifa za kusifu wahalifu, kuzua taharuki
Habari Mchanganyiko

Wanahabari watakiwa kuweka kando taarifa za kusifu wahalifu, kuzua taharuki

Spread the love

VYOMBO vya habari nchini Tanzania, vimetakiwa kuacha kutoa taarifa za kihalifu kwa njia ambazo zinawapa sifa wahalifu, kuumiza wahanga na kuzuia taharuki kwa jamii. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumamosi, tarehe 14 Mei 2022, katika mjadala wa kujadili nafasi ya vyombo vya habari kwenye kuripoti matukio ya kihalifu na haki za binadamu, ulioandaliwa na Chama cha Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), uliofanyika mtandaoni.

Akizungumza katika mjadala huo, Kamishna wa Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi, CP Hamad Hamis Hamad, amevitaka vyombo va habari kutumia vyanzo vya Polisi katika kuripoti taarifa za kihalifu, hususan zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii, ili kudhibiti usambazaji wa taarifa za kughushi zenye kuzua taharuki kwa jamii.

“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa vyombo vya habari kuhamasisha Watanzania kushirikiana na Polisi katika ulinzi wao na mali zao, kwa kutoa taarifa za uhalifu ili kushughulikiwa kabla uhalifu haujatokea na kuleta madhara kwa watu,” amesema CP Hamad.

Naye Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP David Misime, amevitaka vyombo vya habari visiandike habari kwa kukurupuka ili kukwepa taharuki.

“Vyombo vya habari vihakikishe taarifa inazotoa hazikuzi uhalifu zaidi, hazileti hofu kwa jamii lakini pia kuharibu ushahidi na kuwapa wahalifu sifa zaidi. Mfano kusema panya road ambao vijana wadogo wamefunga mtaa. Wanafungaje mtaa wakati wanaume wapo,” amesema SACP Misime na kuongeza:
“Tunatoa wito kwa vyombo vya habari kutoa taarifa ambazo wananchi wanazielewa bila kuathiri upelelezi, ushahidi au kuleta hofu kwa jamii. Mjue taarifa za uhalifu hazina budi kukusanywa, kuchambuliwa na kutolewa kwa makini bila kukurupuka.”

Kwa upande wake Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, ameshauri utafiti ufanyike ili kubaini chanzo cha kuibuka kwa makundi ya kihalifu hasa yanayoundwa na watoto maarufu kama Panya Road.

“Sasa tunazungumza Panya Road, sihani kama kuna utafiti unaofanyika kujua tatizo la Panya Road ni nini. Lazima twende mbali tuangalie kwa nini tunakuwa na watoto wengi wanaojikusanya kuwa Panya Road, tuangalie wamekutana na nini,” amesema Olenguruma.

Naye Mwenyekiti wa OJADACT, Edwin Soko, amevitaka vyombo vya habari vijikite zaidi katikia kutoa taarifa zenye lengo la kuelimisha jamii kuhusu uhalifu, hususani madhara yake ili wahusika waache kutekeleza vitendo hivyo.

“Watu wanatakiwa waelewe jinsi gani uhalifu umetokea, kwa namna ipi uhalifu umetokea ili kuchukua tahadhari na wao kuwa makini ili uhalifu usitokee. Ni vyema kuripoti ili wananchi wachukue tahadhari,” amesema Soko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!