December 4, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanahabari watakiwa kutoandika habari zinazosababisha machafuko

Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile

Spread the love

 

WAANDISHI wa habari nchini, wametakiwa kukwepa kuandika habari zinazoweza sababisha machafuko, ili kulinda usalama wa nchi na haki za wengine. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumamosi, tarehe 22 Oktoba 2022, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akitoa mada katika mafunzo kwa wahariri juu ya mikakati ya uchechemuzi kuhusu marekebisho ya Sheria za habari.

Ni wakati akitoa mada juu ya kanuni za kimataifa kuhusu uhuru wa kujieleza na upataji taarifa.

Mwenyekiti huyo wa TEF amesema katiba ya nchi imetoa haki ya mtu kutafuta, kupata na kusambaza taarifa bila mipaka, lakini imeeelekeza haki hizo zisikiuke haki nyingine.

“Unaweza ukawa na haki yoyote, lakini inapofika mahali unaona inaelekea kuketa vurugu unaiacha. Tu-mantain public order, inapofika Mahali Kuna chaos (machafuko), hata habari iwe nzuri kiasi Gani inabidi uikwepe Ile chaos,” amesema Balile.

Balile amesema “tukienda Ibara ya 28 ya katiba, inasema haki yako inapokomea ndipo inaanzia haki ya mwingine. Japo tulipo Kila mtu anapenda kuzungumza lakini wote wakizungumza Ile haki ya kusikia na kusikika itavunjwa tutakuwa hatusikilizani.”

Balile amesema, hata mikataba ya kimataifa ikiwemo Mkataba wa Haki za Kisiasa na Kijamii (ICCPR), inahimiza taarifa zinazotakiwa kusambazwa Kwa umma ni zile zinalinda haki za wengine na maslahi ya taifa.

Aidha, Balile ameiomba Serikali ifanyie marekebisho Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya 2016, Kwa ajili ya kuweka kifungu kinachoainisha habari zinazopaswa kutoandikwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kuhatarisha usalama wa taifa, uchumi wa nchi na kutia hofu jamii.

“Katika kutunga Sheria na hii ndiyo moyo wenyewe, Kuna kitu kwamba tunapotunga Sheria Kuna masharti makuu matatu ya sheria za kihabari, kwamba habari ziruhusiwe vipi na zinaweza kuzuiliwa vipi. Kama Kuna haki iliyozuliwa iwe na sheria inayozuia yaani isiwe kificho. Sheria inapaswa kutamka habari zilizozuiliwa,”

“Vigezo vya habari kuzuiwa ni kulinda haki za wengine na heshima za watu na kulinda usalama wa nchi,” amesema Balile.

Pia, iondoe kifungu Cha sheria hiyo kinachowanyima fursa raia wa kigeni kupata taarifa kinyume cha mkataba wa ICCPR.

“Tukumbuke tunapopambana na sheria yetu ya kupata taarifa, inasema mtu ambaye si Mtanzania hawezi kupata taarifa lakinj azimio hili linasema Kila mtu ana haki ya kupata taarifa bila kuingiliwa,” amesema Balile.

error: Content is protected !!