July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi watatu wafariki kwa mshituko wa moyo wakati wa mtihani

Spread the love

 

WAKAZI wa Jimbo la Gujarat nchini India , wamepigwa na mshangao mkubwa , baada ya wanafunzi watatu kufariki dunia ghafla, kutokana na mshituko wa moyo sababu ya mtihani. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa mtandao … (endelea)

Wanafunzi anayefahamika kwa jina la Sneh , alipatwa na mshituko ghafla akazimia akiwa kwenye chumba cha kufanyia mtihani , wakati alipokuwa akiandika kwenye karatasi ya mtihani katika shule ya Sekondari ya Limbassi, gari la kubebea wagonjwa liliitwa ili kumpeleka Hospitali kuokoa maisha yake , madaktari waliokuwepo katika hospitali hiyo wamesema kwamba mwanafunzi huyo amekufa kutokana na mshituko wa moyo.

Sambamba na mwanafunzi Sheikh Mohammed Aman Arif, ambaye aliyekuwa katika eneo la Ahmedabad akifanya mtihani alianza kuonesha dalili za kuzorota kwa afya yake kutokana na mtihani aliokuwa akiufanya , Gari la wagonjwa liliitwa na kumkimbiza hospitali ambako aliongezewa Oksijeni lakini alifariki dunia, madaktari wamesema shinikizo la damu yake ilikuwa kiwango cha juu sana.

Mwanafunzi Utsav Shah kutoka shule ya Sekondari Navsari, ni sawa na wenzake yeye alipatwa na mshituko wa moyo kabla la kuanza kufanya mtihani, akiwa nyumani kwao. Watu wa familia yake walimkimbiza hospitali bila mafanikio akiwa na maumivu ya kifua , ambako madaktari walitangaza kuwa amefariki , baba yake alisema kwamba alikuwa na mshituko wa moyo.

Vifo vya ghafla vya wanafunzi hao , waliokuwa wakifanya mtihani wa kitaifa kimewashitua wengi kwa ni haijawahi kutokea miaka.

error: Content is protected !!