January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi waombwa kujiandikisha kupiga kura

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, amewataka vijana wote wanaomaliza masomo ya sekondari kushiriki kikamilifu katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, ili kuwachagua viongozi bora katika uchaguzi mwezi Oktoba mwaka huu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Chikawe ametoa kauli hiyo leo kwenye mahafali ya nne ya kidato cha sita, shule ya St. Joseph iliyopo katika Makao Makuu ya kanisa Katoriki, jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo amesema, vijana wanaomaliza masomo ya sekondari wanakuwa na uelewa wa kutosha juu ya mambo ya siasa nchini kutokana na elimu wanayoipata pindi wakiwa darasani.

Mbali na kuwasihi vijana kushiriki upigaji kura, pia Chikawe amewakanya kutojihusisha katika makundi mabaya ya uharifu pindi wanapomaliza shule, badala yake wawe mfano wa kuigwa kwa jamii kwa kuleta mabadiliko kwa vijana wasioelimika.

“Inasemekana kwamba, makundi mengi ya ugaidi yanaongozwa na wasomi, ambao wamekaa darasani kujifunza vitu vizuri lakini wao wanavigeuza. Matumizi mabaya ya mitandao pia ni chanzo cha vijana wengi kuharibika, hivyo nitoe wito kwa mliomaliza shule hii mkawe mfano mzuri kwa jamii,” amesema Chikawe.

Naye Mkuu wa Shule hiyo, Sista Theodora Faustine, wakati wa kusoma risala yake kwa mgeni rasmi, aliorodhesha changamoto mbalimbali wanazopata wanafunzi, kubwa ikiwa ni ukosefu wa mabweni.

Faustine amesema, licha ya shule hiyo kuwa na sifa ya ufaulu mzuri kwa miaka yote, lakini bado wanachangamoto nyingi zinazowakabili, na kubwa kuliko ikiwa ukosefu wa mabweni ya kudumu kwa wanafunzi hao.

error: Content is protected !!