Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanafunzi waliosimamishwa UDSM, mikononi mwa baraza la nidhamu
Habari Mchanganyiko

Wanafunzi waliosimamishwa UDSM, mikononi mwa baraza la nidhamu

Spread the love

HATIMA ya wanafunzi watano wakiwemo viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) kuendelea na masomo au kufukuzwa iko mikononi mwa baraza la nidhamu la chuo hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wanafunzi hao walisimamishwa masomo na uongozi wa UDSM tarehe 18 Desemba 2019 kupisha uchunguzi wa tuhuma za kukiuka sheria ndogondogo za wanafunzi chuoni hapo.

Waliosimamishwa ni; rais wa Daruso, Hamis Mussa, waziri wa mikopo,Malekela Brington, waziri wa habari, Judith Maliki pamoja na wanafunzi wengine Milanga Hassan na Ititi Mussa.

UDSM ilichukua uamuzi huo baada ya Daruso kutoa saa 72 kuanzia tarehe 15 Desemba 2019 kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutoa mikopo kwa baadhi ya wanafunzi chuoni hapo ambao walikuwa wanadai.

Hatua hiyo ilimfanya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kuutaka uongozi wa UDSM kuchukua hatua dhidi ya wale wote waliohusika kutoa tamko hilo.

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE kwa njia ya simu leo Ijumaa tarehe 8 Mei 2020, Profesa William Anangisye, Makamu Mkuu wa UDSM, amesema suala hilo bado liko katika mchakato chini ya baraza la niadhamu la chuo hicho.

Hata hivyo, Profesa Anangisye amesema hawezi kueleza zaidi hatua iliyofikiwa juu ya mchakato huo, kwa kuwa ni kinyume na taratibu kuzungumzia suala ambalo mchakato wake bado haujakamilika.

“Ungewauliza wanafunzi wenyewe kwamba hilo suala lao limefikia wapi kwa kuwa ndiyo wahusika, mimi siwezi jibu kwa sababu kitu kilicho katika mchakato sio sahihi kulizungumzia zaidi.”

“Tusibiri tufike mwisho. Kesi bado inaendelea haijafika mwisho siwezi kueleza kinachoendelea,” amesisitiza Profesa Anangisye.

MwanaHALISI ONLINE ilimtafuta Mussa na Maliki, kwa njia ya simu, lakini mawasiliano yao hayakupatikana.

Jana Alhamisi, Jackline Ndombele, Kaimu Rais wa Daruso akizungumza na MwanaHALISI ONLINE alisema wanafunzi hao walihojiwa na kamati ya nidhamu kuhusu tuhuma zao, ambapo waliwasilisha utetezi wao kwa njia ya maandishi.

Ndombele alisema baada ya wanafunzi hao kuhojiwa na kuwasilisha utetezi wao, kamati hiyo ilipeleka mapendekezo juu ya suala hilo, kwa baraza la nidhamu la UDSM, ambapo linatarajiwa kutoa uamuzi baada ya kupitia mapendekezo hayo.

Hata hivyo, Ndombele alisema kwa sasa suala hilo limekwama kutokana na vyuo vyote nchini kufungwa kufuatia janga la mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19).

“Kamati ya nidhamu iliundwa na waliitwa na kamati hiyo na kila mmoja alisomewa na kujibu mashtaka yake kwa njia ya maneno na maandishi.”

“Baada ya hapo, kamati hiyo iliwasilisha mapendekezo yake katika baraza la chuo. Lakini bado hawajatoa uamuzi wa mwisho kutokana na vyuo kufungwa kutokana na janga la Corona,” amesema Ndombele.

Tarehe 18 Machi 2020, Serikali ya Tanzania ilitangaza kuvifunga kwa siku 30 vyuo vyote nchini humo ili kujikinga na maambukizi ya corona. Pia, shule zote za msingi na Serikali nazo zilifungwa kwa muda huo kuanzia tarehe 17 Machi 2020.

Hata hivyo, baada ya siku hizo kumalizika, Serikali ilisema vyuo vitaendelea kufungwa hadi pale hali ya maambukizi ya corona yatakapopungua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!